Kampuni ya Mega Beverages Limited (MBL) imeadhimisha miaka 20 ya uwepo wake sokoni kwa kuzindua K-Vant Premium Spirit Special Edition, toleo maalum la msimu wa sikukuu lenye muonekano wa dhahabu na ladha ya kipekee.

Hafla ya uzinduzi wa chapa hii umefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali, akiwemo mgeni rasmi Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi wa TIC, aliyesifu mchango wa Kampuni ya Mega Beverages Limited katika kukuza uchumi wa ndani kupitia bidhaa zake zenye ubora wa hali ya juu.

Naye meneja wa Chapa hiyo, Awatif Bushiri, alisema, ‘K-Vant Special Edition imehamasishwa na uthubutu wa kila siku wa Watanzania, na ari yao ya kutokata tamaa katika kufanikisha kesho iliyo bora. “Tunamkaribisha kila mmoja mwenye umri zaidi ya miaka 18 kufurahia bidhaa hii ya kipekee kabisa”.

Bushiri alisisitiza upekee na mvuto wa bidhaa yenye rangi ya dhahabu, iliyotengenezwa kutokana na mimea safi, yenye ladha murua na harufu ya kuvutia. Alisema toleo hili maalum lenye ujazo wa ml 750 litauzwa kwa TZS 25,000 kote nchini.



Share To:

Post A Comment: