Na Denis Chambi, Tanga.
TAFITI za mwaka 2021 zilizofanywa na shirika la kazi Duniani 'International Labour Organization 'ILO' nchini Tanzani zimebaini kuwa biashara ndogo ndogo zinazofanywa na wajasiriamali wengi na wa kati zimekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo athari zinazowakabiri wanawake licha ya sekta hiyo kuzidi kukua kila mwaka.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa shirika hilo hapa nchini Rukia Lukanza wakati walipokutana na wafanyabiashara wadogo wadogo na wati Mkoani Tanga kwa ajili ya kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa kurasimisha biashara zao ili ziweze kutambulika na mamlaka husika hatua ambayo itakwenda kutatua changamoto zinazowakabili na hatimaye kupata manufaa zaidi
Lukanza amesema kuwa katika kutafuta njia mbadala ili kuweza kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo ambao huchangia uchumi wa Taifa, ILO limepitia miongozo iliyopo hapa nchini ambapo Kwa kushirikiana na Baraza la uwezeshaji kiuchumi wamedhamiria kuwapa elimu watanzania ili kunufaika zaidi na biashara wanazozifanya.
" Kuna utafiti wetu wa Taifa ambao tulifanya kwa mwaka 2021 umeonyesha kwamba biashara ndogo ndogo zisizokuwa rasmi zimekuwa na mapungufu mengi kwanza sekta imeongezeka na kumekuwa na athari ambazo zinawakabili wanawake , kulikuwa na wajasiriamali ambao wanakosa hata zile haki ndogo ndogo za kawaida kabisa"
"Hata hivyo ILO imeipongeza Tanzania kufwatia hatua mbalimbali zilizochukuliwa ikiwa ni miongoni mwa utatuzi wa changamoto katika sekta hiyo ambapo wafanyabiashara wadogo wadogo wameweza kupatiwa mikopo ya asilimia 10 kupitia halmashauri zao pamoja na kuwaboreshea mazingira ikiwemo sehemu rasmi za masoko pamoja na kuwatambua.
"Nitambue na kupongeza juhudi za nchi kwa mafanikio katika kutekeleza ukuaji wa uchumi na katika kutoa fursa ambazo zinasaidaia kupata huduma ambazo zinawezesha watanzania wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wadogo kuzirasmisha biashara zao ambazo hazikuwa rasmi" alisema
Akifungua mafunzo hayo katibu mtendaji wa Baraza la uwezeshaji kiuchumi nchini Tanzania Bengi Issa amesema kuwa kufwatia maboresho yaliyofanywa na Serikali katika sekta ya biashara imekuwa mwarobaini wa changamoto zilizokuwa zianawakabiri wafanyabiashara hususani wadogo wadogo na wakati hivyo kuwaasa kuendelea kurasimisha biashara zao ili waweze kutambulika rasmi.
Ameongeza kuwa kufwatia hatua ya Serikali kutenga asilimia 30 ya manunuzi yake ambayo yameelekezwa kwenda kwa makundi maalumu ya wakina mama, vijana na watu wenye ulemavu ni fursa pekee kwao kupata nafasi ya kuonyesha ufanisi na ubora wabidhaa zao wanazozalisha na kuzipeleka kwa walaji.
"Fursa nyingi zinazotokea kwa wafanyabiashara inategemea na yeye mwenyewe kama amesajiliwa , fursa zozote zinazotokea ndani ya Serikali huwezi kuzipata kama biashara yako sio rasmi"
"Mafunzo haya tutayatoa kwa mikoa Saba na baadaye kueneza kwa nchi nzima nia yetu ni kwamba wafanyabiashara wote waweze kurasimisha ili kunufaika na fursa yeyote ambayo itatolewa na Serikali" alisema Issa.
"Sasa hivi tunafahamu kwamba Serikali imetenga asilimia 30 ya manunuzi yake yaendelee kwenye makundi maalumu ambapo mpaka sasa hatujafika hata asilimia 5 watu bado hawana taarifa na hawana ujuzi ambao unatakiwa sisi kama Baraza la uwezeshaji tutahakikiaha wananchi wanapata hizi fursa" alisema Katibu huyo
Akizungumza mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye pia ni miongoni mwa watu wenye ulemavu amepongeza Serikali kurudisha asilimia 10 ya mapato ya halmashauri ambayo wanapata asilimia 2 huku akiiomba kuendelea kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kibiahara ili kuweza kujiingizia kipato.
"Tunapongeza na kuishukuru Serikali kupitia mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri sasa hivi tunaona mtu mwenye ulemavu hata akiwa mmoja anaweza kupata mkopo niwaombe haya maboresho yanayotolewa tuendelee kuitwa tuelimishwe"
Mafunzo hayo ya urasimishaji wa biashara yamelenga kuwafikia zaidi wajasiriamali ili kupata elimu juu ya utendaji na uboreshaji wa biashara zao na hatimaye kujipatia kipato yatafanyika katika mikoa 7 ya Tanzania ambayo ni Tanga, Mwanza , Kagera, Shinyanga , Tabora Kigoma na Ruvuma.
Post A Comment: