Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA wameibuka mabingwa katika michezo mbalimbali ambayo wanafunzi wameshiriki katika mashindano yanayohusisha Vyuo vya Elimu ya juu (SHIMIVUTA) yaliyokuwa anafanyika katika uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Akifunga mashindano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimajaro Kiseo Yusuf Nzowa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema michezo ni afya, michezo ni furaha lakini pia michezo huleta umoja na mshikamano, hivyo ni vyema vijana wa vyuo na wengine wote waendelee kushiriki ili kujenga umoja huo na mshikamano kwa taifa.
Kwa upande wake Meneja wa Kampasi ya Arusha IAA Dkt. Grace Temba amewapongeza wachezaji na wanafunzi wote wa IAA walioshiriki katika mashindano hayo na kusisitiza kuwa wameiheshimisha taasisi kwa kuibuka washindi wa jumla (overall winner) katika mashindano hayo.
Dkt. Grace amesisitiza Menejimenti ya IAA inayoongozwa na Prof. Eliamani Sedoyeka kwa ujumla wamekuwa na desturi ya kusapoti sekta ya michezo na watahakikisha wanaendelea kuweka nguvu katika kukuza vipaji vya wanafunzi kwa manufaa ya Chuo na taifa kwa ujumla.
Chuo Cha Uhasibu Arusha kupitia wachezaji wake kwenye michezo tofauti tofauti kimefanikiwa kuchukua makombe na medali mbalimbali kama ifuatavyo
-Bingwa wa jumla wa mashindano
-Bingwa mpira wa miguu kwa wanaume
-Kocha bora wa mashindano mpira wa miguu kwa wanaume
-Mlinzi bora wa mashindano mpira wa miguu ---Mshindi wa kwanza mchezo wa kuvuta kamba wanaume na wanawake
-Mshindi wa kwanza mbio za kijiti kwa wanaume na wanawake
-Mshindi wa pili mchezo wa pool table
-Mshindi wa kwanza riadha Mita 200 kwa wanawake
-Mshindi wa pili riadha Mita 200 kwa wanaume
-Mshindi wa pili riadha Mita 100 wanaume na wanawake
-Mshindi wa kwanza mchezo wa rede kwa wanawake
Mashindano hayo yaliyodumu kwa takribani wiki mbili yametamatika leo rasmi katika Uwanja wa Ushirika Stedium Moshi na jumla ya Vyuo ishirini vya Elimu ya juu Tanzania vimefanikiwa kushiriki.
Post A Comment: