Mbunge wa jimbo la Babati mjini Pauline Gekul amefanya ibada ya kutoa shukrani kwa Mungu kwa changamoto mbalimbali alizopitia mwaka huu 2024 ikiwemo sakata la kutuhumiwa kumuingizia chupa sehemu ya haja kubwa kijana aliyefahamika kwa jina la Hashimu jambo ambalo amesema hakulifanya kabisa.


Ibada hiyo ya shukrani aliyoifanya katika kanisa la kiinjili la kilutheri KKKT lililopo Babati mjini Gekul amesema ni sehemu ya kupata faraja na kumrudishia Mungu shukrani kwa mapito magumu aliyopitia na kusema ni muda sasa wa wananchi kujua ukweli uliopo na kuacha kumnenea mabaya.

“Leo nimeshukuru kanisani na nadhani kuendelea kuhukumiwa kilasiku kwa masuala ya uongo si sahihi watu wajue ukweli, kwasababu kwa mwaka mzima huu wakati natuhumiwa watu wakiongea kama sio maombi yenu viongozi wa dini mimi binafsi nisingeweza kuishi tena.”

Aidha Gekul amesema ni dhahiri kuwa Mungu amemjibu maombi yake kwani hata ripoti ya kitabibu baada ya vipimo imeonesha wazi kuwa kijana huyo hakuwa na majeraha yeyote kwenye mwili wake wala dalili zozote za yeye kuingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa na hata alivyofika kituo cha polisi alieleza kuwa amepigwa na mtu asiyejulikana, sasa ameamua kuyasema hayo ili watanzania wote wajue ukweli na kupunguza maumivu mazito aliyoyabeba tangu jambo hilo lilipozushwa.

“Walivyofika polisi, huyo kijana akasema amepigwa na mtu asiyejulikana, kwanini hawakwenda na kusema Paulina ndo amewapiga na kuwadhuru? Nimeona mwaka huu wakati namaliza nimshukuru Mungu moyo wangu niukung’ute niseme kila kitu ili na mimi nisiendelee kutembea kama roboti na kulia moyoni.”




Share To:

Post A Comment: