Angela Msimbira RUVUMA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango ametoa rai kwa wadau wa maendeleo na taasisi binafsi kutoa elimu kuhusu maambukizi ya virusi
vya ukimwi kuanzia ngazi binafsi, familia na jamii kwa ujumla ili kuondoa mitazamo hasi uliopo katika jamii.
Ametoa rai hiyo leo Disemba 1,2024 kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Majimaji Mkoani Ruvuma.
Dkt.Mpango amewataka wananchi wote nchini kuzingatia maudhui ya elimu inayotolewa kupitia kampeni mbalimbali kwa ajili ya kubadili tabia, kuachana na mila na desturi zinzoweza kuwa kichocheo cha maambukizi na kuendelea kijikinga na maambukizi mapya ya viriusi vya ukimwi.
Ameendelea kufafanua kuwa kasi ya maambukizi katika kundi la vijana imeongezeka ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kundi la vijana hasa watoto wa kike ndio liko kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya ya vvu
Aidha, ametoa rai kwa Tume ya kuthibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) kushirikiana na wizara za kisekta, wadau na jamii kwa ujumla kuweka mkazo katika kudhibiti mazingira yanayochochea maambukizi ya vvu
Amewataka vijana kujitambua, kujidhamini na kutunza maisha yao kwa kujikinga na maambukizi mapya ya VVU na kuwasihi wale wanaoishi na virusi vya ukimwi kuendelea kutumia dawa za ARV kwa usahihi ili kufubaza makali ya virusi.
Post A Comment: