Na Fredy Mgunda, Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe Victoria Mwanziva amewasisitiza wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA Wilaya ya Lindi kusimamia ubora na thamani ya fedha kwenye ujenzi wa Mradi wa barabara ya Mtange - Kineng'ene yenye urefu wa Mita 600 unaojengwa kwa kiwango cha lami leo hii Tarehe 20/12/2024
DC Mwanziva ametoa wito huo alipofanya ziara ya kukagua uendelevu wa mradi wa barabara hiyo, ambapo amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kushusha 449,897,000/= kwa ajili ya mradi wa Barabara ya Mtange-Kineng’ene Wilayani Lindi.
DC Mwanziva amegusia namna ambavyo Serikali imeendelea kutoa Fedha kwa ajili ya matengenezo na maboresho ya Barabara Katika Wilaya ya Lindi, ambapo kwa sasa Bajeti imeongezeka kutoka wastani wa bilioni mbili kwa mwaka Hadi kufikia Bilioni nane kwa mwaka 2024/2025.
Mhandisi Dowson Pascal- Meneja wa TARURA Wilaya ya Lindi amesema Mradi huo wa barabara wa mtange - Kineng'ene unaogharimu kiasi cha Tshs 449,897,000/= unatekelezwa kw ufanisi na hadi sasa umefikia 70% ya utekelezaji wake huku mkandarasi wa Mradi huo aliahidi amejipanga kukamilisha mradi kwa wakati.
Katibu wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini Asha Mwendwa amesisitiza Mradi huo kukamilika kwa wakati kwani unahudumia wananchi wengi wanaoishi Kineng’ene, Milola, Matimba, Chikonji na Nangaru hivyo ni tegemeo na litazidi kuchagiza Uchumi na uchukuzi kiujumla.
Post A Comment: