Katibu Tawala (W) Kasulu Theresia Mtewele akiangalia mpango wa ujenzi wa madarasa 
Katibu Tawala (W) Kasulu Theresia Mtewele akiangalia mpango wa ujenzi wa madarasa

Na Fredy Mgunda, Kasulu, Kigoma.

Katibu Tawala (W) Kasulu Theresia Mtewele amesisitiza kulipa fidia kwa wakati katika maeneo ya wananchi ambao wamepisha ujenzi wa miradi ya maendeleo.


Hayo ameyasema wakati  akifanya majumuisho mara baada ya ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kutembelea miradi ya Kasulu Mji.


Mtewele amesema ulipaji wa fidia kwa wakati unatoa hamasa kwa wananchi kutoa maeneo yao pindi yanapoitajika kuweka miradi mbali mbali.

“Tunaju kama tuna maeneo yetu lakini ipo miradi mingine itahitaji maeneo ya wananchi kwa hiyo unapolipa fidia kwa wakati unahamadisha na wengine kukubalinkwa haraka kutoa maeneo yao kupisha miradi.”


Pia amewataka wahusika wote wanaopelekewa miradi kuitunza na kuzingatia usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuleta unadhifu hususani maeneo ya hospitali.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mji Kasulu Mwl. Vumilia Julius Simbeye amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na wajumbe wa Kamati hiyo na kuyatekeleza ili kuhakikisha miradi inakua yenye tija kwa wananchi.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: