Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati Chuo hicho,jijini Arusha.
Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimesema kuwa mikakati yake kwa wahitimu kutengeneza ajira na sio kutafuta ajira kutokana ufundishaji wanafunzi katika kubuni miradi ambayo inaanzwa kuendelezwa chuoni.
Hayo ameyasema Profesa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Chuo jijini Arusha.
Amesema kuwa Chuo kimechukua jitihada za tofauti katika uandaji wa wanafunzi wanapohitimu wanakuwa kitu cha kufanya na sio wanahitimu wanakaa kusubiri ajira.
Profesa Sedoyeka amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imwekeza nguvu katika shule za Msingi na Sekondari ambapo wanafaulu kwa ajili ya kujiunga na Vyuo hivyo lazima waandaliwe vyema katika kuwa suluhisho ya changamoto katika jamii ambayo kwao ni fursa ya ajira.
Amesema kuwa Chuo kimekuwa kikikua kwa kasi kutokana na kupokea wanafunzi wengi kutokana na kuanzisha kozi ambazo zimetafitiwa zinaweza kubadili mtazamo wa wanafunzi katika soko la ajira la kuwa sehemu ya wazalishaji wa ajira.
Aidha amesema kuwa wanafunzi wenye mawazo ya ubunifu wameweza kuendelezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kampuni na kusajiliwa katika mamlaka za usajili nchini.
Profesa Sedoyeka amesema katika mikakati mingine ni kwenda kimataifa kwa kuwa vyuo katika nchi za Sudani Kusini pamoja na Comoro kutokana na Teknolijia ya Tehama Mhadhiri kufundisha huko kwa njia ya mtandao.
Amesema katika jitihada hizo wameshasaini mikataba ya makubaliano mitano hiyo imetokana na uwezo wa Chuo kujitosheleza kwenda kimataifa katika kufanya mashirikiano ya nchi Uingereza pamoja na China
Hata hivyo amesema kuwa katika ujenzi na maboresho ya Chuo hicho watakuwa na maduka ambapo wanafunzi watafungua ofisi zao na baada ya kukua wanaondoka na kuingia wengine lengo kuangalia maendeleo yao.
Profesa Sedoyeka amesema kuwa katika kujitanua wameanzisha vyuo na kuanza kujenga vyuo katika Mikoa ya Dodoma,Babati,Songea huku Dar es Salaam na Arusha vikiendelea katika kuboreshwa.
Amesema kuwa kilianza na wahadhiri wa shahada ya uzamivu Saba lakini sasa wamefika 38 huku wengine 88 wakisoma shahada hiyo.
Profesa Sedoyeka amesema kuwa katika makitaba wamekwenda na teknolojia ya Tehama ya wanafunzi kupata vitabu katika mtandao wa chuo na imesaidia kupunguza mahitaji ya vitabu.
Msimamizi wa Kituo cha Kiotamizi wa (IAA) Sarah Adamson Amesema kuwa katika usimamizi wa mawazo bunifu ya kibiashara kwa wanafunzi imekuwa na matokeo chanya kwa vijana wanavyohitimu wanakuwa ajira zao.
Amesema kuwa wanafunzi wamekuwa wakipata ushindi wa mawazo yao ambapo inawasaidia kupata fedha.
Jengo la Kisasa linalojengwa katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)
Post A Comment: