Na Fredy Mgunda, Iringa.
Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimempa tuzo ya shukurani mjumbe wa Halmshauri kuu ya CCM taifa (MNEC) Salim Abri Asas kwa mchango wake mkubwa ndani ya chama hicho mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla.
Akikabidhi tuzo hiyo mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Ndugu Daudi Yassin, amesema chama kinamshukuru na kinatambua mchango wa Asas wa hali na mali kwa chama hicho, na kwamba kinathamini na kimeamua kumpa tuzo hii ya shukrani.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, MNEC Asas amewashukuru viongozi wa CCM Mkoa wa Iringa kwa kutambua mchango wake na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za chama. Pia, amewashukuru wananchi kwa kuendelea kukiamini chama cha Mapinduzi, huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa ndani ya chama hicho na taifa kwa ujumla.
Post A Comment: