Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Bwanku Bwanku ameendelea kugawa mipira kwa timu mbalimbali za Kata ndani ya Tarafa ya Katerero ikiwa ni hatua ya kuunga mkono mkakati wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuinua michezo na kukuza ajira zaidi kwa Vijana kupitia michezo. 

Na Fredy Mgunda,Bukoba,Kagera.

Mpaka sasa wanku amegawa mipira kwenye timu za Kata ya Kishogo, Ibwera, Kemondo, Katerero huku taratibu za kugawa kwenye Kata zingine zikiendelea.

Hizi ni jitihada za makusudi za Bwanku kumuunga mkono Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyedhamiria kuinua michezo nchini kwa vitendo na si maneno. Tayali Serikali ya Rais Samia kwa muda mfupi imeongeza Bajeti ya michezo kwa zaidi ya mara 8 kutoka Bilioni 35 tu hadi sasa imefika Bilioni 285, kujenga Viwanja vya Kisasa vya michezo mkoani Dodoma na Arusha, kuvipa motisha vilabu vyetu na Timu ya Taifa ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania Yanga na Simba vilifika Roba Fainali Kombe la Afrika kwa mwaka mmoja na mengine mengi.

Bila kusahau Serikali ya Rais Samia ilifanikisha kupatikana kwa mipira zaidi ya 1,000 kutoka FIFA kupitia TFF na kuigawa kwenye shule mbalimbali mikoa yote Tanzania ili kuinua michezo. 

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

mwangaza wa hbari

Post A Comment: