Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Abdul Omary Nondo amepatikana usiku huu baada ya kutupwa karibu na Makao Makuu ya Chama hicho Magomeni Jijini Dar es salaam akiwa na majeraha.


Taarifa za awali kutoka ndani ya ACT Wazalendo zinasema Nondo ambaye alitekwa leo asubuhi katika stendi ya Magufuli Mbezi Luis Jijini Dar es salaam akitokea Kigoma, amepatikana akiwa na majeraha ambayo yametokana na vipigo na sasa anapelekwa Hospitali akiwa mahututi.
Share To:

Post A Comment: