Na.Ashura Mohamed - Arusha

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeanzisha mfumo maalumu wa kielektroniki mahususi kwa ajili ya kushughulikia changamoto na malalamiko ya wateja kuhusiana na huduma za kibenki.

Mfumo  huo utazinduliwa Januari 2025 ambapo utawezesha mteja kuweza kupata huduma kidigitali na kwa wepesi huku ikiokoa  muda na gharama ambapo hapo awali hapakuwa na namna ya kuona kushughulikia changamoto. 

Akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili Meneja Uchumi kutoka Benki Kuu Tawi la Arusha (BOT) bw.Aristedes Mrema alisema kuwa warsha hiyo ya siku mbili ni matumizi ya mfumo wa kielektroniki ya utatuzi wa malalamiko ya fedha .

"Benki kuu ina jukum kubwa la kuhakikisha kuwa inalinda watumiaji wa huduma ya wateja wanaokopa na kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora kwa kuzingatia sheria za fedha "Alisema Bw.Mrema

Aidha alisema kuwa mfumo huo bado haujapatiwa jina rasmi huku ukiwa kwenye majaribio unatarajia kuanza kutumika katikati ya Januari, 2025 ambapo pamoja na mambo mengine unatarajia kurahisisha ufuatiliaji wa malalamiko na kutatuliwa kwa uharaka.

"Kutokana na changamoto mbalimbali ambazo wateja walikuwa wakipata kutokana na kushughulikia wa changamoto zao tunafikiria kuanzisha mfumo wa kielektroniki ambao utaenda kuondoa au kutatua changamoto zao," Alisisitiza Mrema

Pia alisisitiza kuwa hapo awali mteja alikuwa anatakiwa aandike barua kisha ailete kwenye ofisi za Benki Kuu ili malalamiko yake yashughulikiwe lakini pia kulikuwa na changamoto katika ufuatiliaji wa hatua gani utatuzi wa tatizo lake umefikia.

Kwa Upande wake Watoa huduma za akiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya Manemane  Micro Credit iliyopo  mkoani Kilimanjaro bw.Anselimu Peter alisema kuwa mfumo huo utawawezesha wao kama watoa huduma za fedha kufanya kazi kwa kufuata sheria hata mteja anapotoa malalamiko kuweza kuwa na ushahidi wa kutosha.

"Malalamiko yote ya wateja yatakuwa kwenye mfumo itakuwa rahisi pia kufanya rejea kwenye mfumo kuliko kwenye makaratasi kwahiyo tunaamini kwa mfumo huu huduma za kifedha kwa wateja zinaenda kuboreshwa zaidi, kujenga ujasili na uaminifu kwa watumiaji na watoaji wa huduma za kifedha,"Alisema Anselimu 

Nae Bi.Imelda Mathew ambaye ni Mkurugenzi  wa kampuni ya Cas Microfinance Limited iliyopo wilayani Monduli alisema mfumo huo muhimu kwa watumiaji kwa kuwa unaokoa muda gharama  na kuwawezesha kuondoa sababu zisizo za msingi.





Share To:

Post A Comment: