Na Mapuli Kitina Misalaba
Hatua ya robo fainali ya Ligi ya Makamba Lameck (Krismas Cup) imeendelea leo katika uwanja wa Mhangu, kata ya Salawe, ambapo Beya FC imeibuka mshindi kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ikonongo FC maarufu kama Mahakama na kwamba goli hilo pekee limefungwa na nyota wa mchezo huo Bwana Mussa Lukaku.
Akizungumza kwa niaba ya msimamizi wa ligi hiyo, Placid Thomas amesema kesho Jumatatu ligi hiyo haitaendelea kutokana na maadhimisho ya Siku ya Uhuru yatakayofanyika katika uwanja huo kimkoa.
Hata hivyo, ligi itaendelea tena Jumanne kwa mechi nyingine ya robo fainali kati ya Mahando FC na Mwasenge FC, huku Salawe FC na Mwabenda FC wakitarajiwa kuchuana Jumatano ili kukamilisha hatua ya robo fainali na kuingia nusu fainali.
Wachezaji, makocha, na mashabiki wa ligi hiyo wameendelea kumpongeza mdhamini wa mashindano hayo, Makamba Lameck, kwa juhudi zake za kukuza michezo na kuimarisha afya kupitia ligi hiyo.
Ligi ya Krismas Cup, inayodhaminiwa na Makamba Mussa Lameck kupitia kampuni yake ya MCL inayojihusisha na biashara ya nafaka, inalenga kukuza vipaji vya michezo na kuchochea maendeleo ya kimichezo mkoani Shinyanga.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 17 Desemba 2024 ambapo mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapata zawadi.
Placid Thomas, akizungumza kwa niaba ya msimamizi wa ligi ya Krismas CUP.
Placid Thomas, akizungumza kwa niaba ya msimamizi wa ligi ya Krismas CUP.
Post A Comment: