Picha ya pamoja Beya FC kutoka Salawe washindi wa mechi ya leo.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Ligi ya Makamba Lameck maarufu kama Krismas CUP inaendelea kwa kasi katika uwanja wa Mhangu, ambapo leo Beya FC ya Salawe imeibuka mshindi dhidi ya Ngubalu FC ya Mwanza kwa bao moja la pekee lililofungwa na Robert Clement dakika ya 37.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Makamba Mussa Lameck kupitia kampuni yake ya MCL inayojihusisha na biashara ya nafaka, yamelenga kuibua vipaji vya michezo mkoani Shinyanga huku yakichangia mshikamano wa kijamii.

Akizungumza baada ya mechi, Mwenyekiti wa Sungusungu wa kijiji cha Songambele, kata ya Salawe, Moto Mussa Kalamji, amepongeza juhudi za kuandaa ligi hii ambapo ameeleza kuwa mashindano hayo siyo tu burudani kwa wakazi bali pia ni jukwaa muhimu la kuinua vijana wenye vipaji.

“Ligi hii ni fursa ya kipekee kwa vijana kuonyesha uwezo wao. Michezo ni sehemu ya ajira na maendeleo, hivyo nawahimiza wachezaji wote kujituma zaidi,” amesema Moto huku akiwahakikishia usalama wa wananchi katika mashindano hayo.

Msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Emmanuel Enock Kijida, amefafanua kuwa mechi inayofuata itazikutanisha timu za Ikonongo FC na Mwawile FC kesho.

Ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kufurahia michezo na kuunga mkono juhudi za kuendeleza vipaji vya vijana.

Mwenyekiti wa Sungusungu wa kijiji cha Songambele, kata ya Salawe, Moto Mussa Kalamji, akipongeza uwepo wa ligi hiyo huku akiwahakikishia wananchi usalama.

Msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Emmanuel Enock Kijida, akizungumza leo Disemba 3, 2024.

Mechi ikiendelea.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: