Mwanamke mmoja mkazi wa kitongoji cha majengo kijiji cha Magugu wilayani Babati Mkoani Manyara, Juliana Obed (44), amefariki Dunia kwa kung’atwa na nyoka baada ya kuchelewa kulipa shillingi laki moja na nusu (150,000 ) kwaajili ya matibabu.
Akizungumzia tukio hilo mume wa marehemu Obed Meiguani Lazier (50), amesema mkewe alin’gatwa na nyoka Desemba 15, 2024 alipokuwa anachuma boga kisha alimpeleka katika kituo cha afya cha Magugu lakini alishindwa kutibiwa baada ya kushindwa kulipa kiasi hicho cha cha fedha ambacho aliambiwa alipe ili apatiwe matibabu hali iliyomlazimu kwenda kuitafuta lakini alifanikiwa kupata laki na elfu thelathini 130,000 , ndipo mkewe akaanza kuhudumiwa na alifariki baada kuchomwa sindano ya kuzuia sumu isisambae mwilini wakati huo muda ulishaisha na sumu hiyo ilishasambaa.
Kwa upande wao watoto wa marehemu Abedinega Obed na Yona Laizer wamesema kabla mama yao hajafariki alisema ameng’atwa na nyoka mkononi na kuonyesha mikono yake ambayo ilishaanza kuvimba baada ya sumu kuanza kusambaa mwilini nakusema waaguzi wa kituo hicho walishindwa kumhudumia kwa kutanguliza maslahi mbele badala ya utu ambapo wameiomba serikali kuchukua hatua kutokana na tukio hilo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji cha Magugu Loya Amosi amesema tarifa hizo amezipokea kwa mshituko huku akilaani tuko hilo na kuahidi kuchukua hatua stahiki kutokana na mgonjwa kutokupatiwa matibabu nakusema amekwisha wasiliana na mganga mfawidhi wa Kituo hicho.
Naye Mganga mfawidhi wa Kituo cha Afya cha magugu Dkt Kusta Ndunguru amesema taarifa hizo amezipata akiwa safarini na kukiri kwamba alipigiwa simu na mume wa marehemu akimuuliza kuhusu kiasi cha pesa alizoambiwa alipe kituoni hapo ila hakumwambia kama amekwamwa kulipa pesa.A
"Inawezekana kifo cha mama huyo kimesababishwa na kucheleweshwa kupelekwa kituo cha afya,ila nitafuatilia tukio hilo kwa daktari aliyekuwa zamu" alisema Mganga huyo ambaye amedai yupo safarini
Post A Comment: