Na Denis Chambi, Tanga.
KATIBU mstaafu wa Baraza la vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo 'CHADEMA' Mkoa wa Tanga Hemed Said amekana madai ya viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya wanaomtuhumu kukihujumu chama wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika November 27,2024.
Tuhuma hizo dhidi yake zinakuja baada ya Said kushiriki katika kikao cha pamoja na viongozi wa kisiasa wilayani Tanga ambapo Kwa pamoja walipongeza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa , vijiji na vitongoji pamoja na wajumbe ambapo yeye alishiriki kama mgombea licha ya kuwa alienguliwa baada ya kukosa sifa ya kukidhi vigezo.
"Kuna sintofahamu zimetokea Mimi kama mwanasiasa ambaye najifahamu najitambua na ninaelewa chama kina nituhumu kwamba ninahusika moja kwa moja katika kuhujumu mipango ya chama kuhisika na tuhuma hizo ambazo wameziona lakini niwatoe wasiwasi kuwa kuwa mimi sihusiki na hizo tuhuma kwa sababu Mimi ni mstaafu siwezi kuingia kwenye chama kwa njia yeyote bila kufuata taratibu za kichama"
Kufwatia tuhuma hizo Said amebainisha kuwa amekuwa akipata anahifia hali yake ya kiusalama kutokana na kupata vitisho kwa baadhi ya watu wakiwemo viongozi na wanachama wa chama chake hali ambayo imemfanya kuwa na Mashaka.
" Ninapata wasiwasi kwa sababu ninapata vitisho kwa baadhi ya wenzangu wakiwemo viongozi na wanachama changu kwamba ninahusika sasa napata wakati mgumu kuishi Mimi sihusiki na namna yeyote ya kukihujumu chama hiyo naomba Mimi nijivue na sihusiki kwa sababu nipo ndani ya chama kwa zaidi ya miaka 15 nafahamu taratibu miongozi na kanuni zinazohusu uendeshaji wa chama" alisema Said.
"Tukio la mimi kwenda kwenye kikao cha pamoja na viongozi wa kisiasa nilienda kama mgombea ambaye nilienguliwa kwahiyo maoni niliyoyatoa ni kama mgombea aliyeenguliwa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa sasa Mimi ninahusikaje na tuhuma za kuuza au kurubuni mipango au kukwamisha shughuli zozote za mafanikio ya chama changu" alihoji Said.
Aidha amesema kuwa licha ya kupokea vitisho kutoka kwa viongozi na wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA hakukuwepo na utaratibu wowote wa kichama ambao uliofuatwa ikiwemo kumuita kwa nia ya barua.
Kiongozi huyo mstaafu wa Baraza la vijana 'BAVICHA' Mkoa wa Tanga amesema alishiriki kikamilifu mchakato mzima wa uchaguzi kujisaidia chama chake kusaidia kuwapatia wagombea ambao watakwenda katika uchaguzi wa Serikali za mitaa , vitongoji na vijiji.
" Tofauti zozote zinazozungumzwa kwamba Mimi nimehusika kukitubuni chama hizo sio za kweli kwa sababu nimeshiriki ndani ya chama ngazi ya wilaya kutafuta wagombea na mimi nikiwa ni mgombea wa mtaa ambao ninaoishi sasa nahusikaje kukihujuma chama ? hii haiwezekani nasikia wengine wanasema nimenunuliwa sio kweli Nina maisha yangu ninajiendesha kila mtu anafahamu kwa sababu nina uchumi wangu binafsi" alisisitiza mwanachama huyo.
Ameeleza kuwa CHADEMA wilaya ya Tanga kwenye uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji iliweza kusimamisha wagombea 50 lakini wapo 8 ambao walijitoa wakati mchakato huo ikiendelea licha ya kukidhi vigezo alihoji kuwa wamechukuliwa hatua gani tofauti na yeye ambaye alienguliwa kikanuni.
"Ndani ya chama chetu katika halmashauri ya Jiji la Tanga ambayo tuna mitaa 181 tulikuwa na wagombea 50 lakini 8 katika hao tulikuwa na mawakala 182 , je kwanini hawa 8 na Mimi na Hawa ni nani amerubunika , kama walijitoa chama kimewachukulia hatua gani mpaka mimi nionekane kama ninahusika moja kwa moja? Alihoji.
Alieleza kuwa tangu alipojiunga na chama hicho akiwa shule ya Sekondari na baadye kupata nafasi ya uongozi wa Baraza la vijana 'BAVICHA' Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa vijana ambao walisimama kidete kukiteme chama hicho hivyo kuhusishwa na tuhuma za kukihujumu chama chake inampa wakati mgumu.
" Chama kinafahamu kuwa katika vijana ambao walisimama na kupambana kwaajili ya kukisimamisha chama Mimi ni mmoja wapo kwa sababu Nina nafasi yangu kuanzia ngazi ya chuo nimehusika kwenye project nyingi mpaka kwenye ushindi wa ubunge ambao tulipata 2015." Alisema.
Kufwatia hali hiyo Said amesema kuwa atawaandikia barua viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya kisha kupeleka nakala ngazi ya Taifa ili kidai haki yake kama mwanachama halali wa chama hicho.
Alisisitiza kuwa kila mwananchi anauhuru wa kujiunga na chama chochote na kuwa mwanasiasa ambaye anaweza kusimamia maslahi ya wananchi pamoja na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
"Kuchagua chama chochote cha siasa ni utashi wa mtu binafsi kwa sababu wakati ninajiunga na CHADEMA hakuna mtu ambaye alinilazimisha tupo katika harakati kwaajili ya kuwasaidia wananchi popote pale ambapo upo uwatetee wananchi sauti ya wananchi kupitia wewe isikike
Post A Comment: