Kampuni ya Airtel Tanzania imeingia Ushirikiano wa Kimkakati na GSM Haier Tanzania, mpango ambao unalenga kuunganisha Teknolojia itakayoweza kuleta Suluhisho katika matumizi ya Intaneti na kukidhi mahitaji ya sasa ikiwemo kuboresha maisha ya Watanzania.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Disemba 10, 2024, wakati wa Kuingiwa kwa makubaliano hayo Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Tanzania Joseph Muhere, amesema mpango huo pia unalenga Kuzileta pamoja Teknolojia mbili zinazofanya kazi pamoja kwenye makazi.

"Tunawapa fursa pana Watanzania namna bora ya kufurahia urahisi na Maisha ya Kisasa kwa kuunganisha Mtandao wetu wenye kasi na kuaminika wa 5G na Vifaa Bunifu vya Haier, ambapo pia tunalenga kukamilisha lengo la kurahisisha maisha kwa Bidhaa za Kidijitali" amesema Muhere.

Nae Mkuu wa Kitengo cha  Biashara kutoka Haier Tanzania Ibrahim Kiongozi, amesema Teknolojia Bunifu imejikita zaidi kuonesha namna ambavyo Tanzania kama nchi inaendelea kukua katika Suala zima la Teknolojia hasa za kwenye makazi.





Share To:

Post A Comment: