Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kasikazi Pemba na Unguja (Zanzibar) ya kutembelea maeneo ambayo waheshimiwa  wabunge wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walimuomba afike na kujionea changamoto ya Mawasiliano katika majimbo yao.

Mhe. Mahundi amepokelewa na mwenyeji wake Mhe. Dkt Khalidi Salumu Mohammed Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi  wa Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar.

Aidha, Mhe Mahundi katika Ziara hii ametembele maeneo mbali yenye changamoto za mawasiliano Kwa upande wa Mkoa wa Kasikazini Pemba amekagua hali ya mawasiliano katika Kisiwa cha Kojani, Shehiya ya Masota, Kinyikani na katika Jimbo la Mtambwe Kijiji Cha Kidundo pamoja na Wete mjini.

Vilevile, Kwa upande wa Unguja Mhe. Mahundi amekagua hali ya mawasiliano katika maeneo ya kisiwa cha Tumbatu, ametembelea Radio Jamii ya Tumbatu FM , ujenzi wa mnara wa mawasiliano wa Honora katika  shehiya ya Kibuteni









Share To:

Post A Comment: