Na Denis Chambi, Tanga.
SERIKALI Mkoani Tanga imewapongeza wananchi wanaofanya shughuli zao za wavuvi katika bahari ya Hindi ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa pato la Mkoa ambapo huchagia kiasi cha Bilion 5 Kila mwaka.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati akihitimisha kilele cha siku ya mvuvi duniani zilizofanyika Mkoani hapa ambapo amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wavuvi hao huku akiwapongeza baada ya kuachana na masuala ya uvuvi haramu kufuatia kampeni yake aliyoianzisha ya kuwataka kuzisalimisha nyenzo walizokuwa wakizitumia hapo awali.
Katika kuhakikisha Serikali inawawekea mazingira rafiki wavuvi waendelee kunufaika na mazao ya bahari pamoja na kuchangia pato hilo Dkt. Buriani amesema kuwa Serikali inatarajia kutoa boti 4 zitakazotolewa na Mkoa huo huku nyingine 34 zikitarajiwa kutolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Rais alishatanguliza boti 14 na waziri wa uvuvi akaongezea boti 4 na hivi karibuni Mkoa utatoa boti 4 lakini kuna boti 34 atakapokuja Rais wetu zitakabidhiwa kwenu rasmi lakini tutaendelea kumlilia kwamba tunahitaji meli kubwa ambayo itawafanya wavuvi waende katika maji makubwa, kuwe na deep sea fishing waweze kwenda na vifaa vya kutengeneza samaki ili uvuvi wetu uweze kufanyika hata wakati ambao sio mzuri " aliongeza Balozi Buriani.
"Tangu mliporejesha nyenzo haramu mlizokuwa mkitumia kufanya shughuli za uvuvi sasa tuna miezi nane hadi leo hakuna tukio lolote la uvuvi haramu ambao umefanyika mpaka sasa tunajua kwa kuamua kufanya uvuvi halali mmeendelea kupata changamoto kwa sababu bado mna uhaba wa vifaa na bado sekta hii inahitaji kushikwa mkono"
"Tanga tuna wavuvi elfu 13 lakini ni wavuvi hawa wadogo ambao wanatoa mchango mkubwa katika pato la Mkoa na payo la Taifa katika mwambao wetu wa Kilomita 180 ya ukanda wa bahari nyinyi wavuvi wadogo mnachangia Bilion 47 sio fedha kidogo mnapaswa kupongezwa sana mchango huu ni mkubwa, kwa mwaka mnachangia Bilion 5 katika pato letu la mkoa" alisema Dkt. Batilda.
Akizungumza kwa niaba ya katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na uvuvi, Omari Mohammed alisema kuwa sekta ya uvuvi imefanikiwa kuzalisha tani 40,579 ya mazoa yatokanayo na Baharizikiwa na thamni ya shilingi Trillion 2.94 ikilinganishwa na tani 426,505 zenye thamani ya shilingi Trillion 2.86 ikiwa ni ongezeko la 0.61 kutoka mwaka 2023.
Aliongeza kuwa sekta hiyo inaendelea kuhifadhi na kuongeza utalii wa fukwe ili kuendelea kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi huku Wizara ikiendelea na mpango wa kujenga bandari ya uvuvi katika Kilwa Masoko Mkoani Lindi pamoja na ujenzi wa masoko Saba ya mazao yayokanyo na uvuvi pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vinne vya ukuzaji maji.
"Sekta inaendelea kuhifadhi rasilimali za uvuvi na kuendelea utalii wa fukwe kupitia kitengo cha bahari na maeneo tengefu, Wizara inendeleza miundombinu ya uvuvi ikiwemo ujenzi wa Bandari ya uvuvi iliyopo Kilwa pamoja na ujenzi wa masoko Saba ya mazao ya uvuvi na mialo mitatu ya kupokelea samaki pamoja na kukamilisha ujenzi vituo vinne vya ukuzaji maji"
Ameongeza kuwa sekta ya Mifugo na uvuvi kwa mwaka huu inaendelea kutekel za vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na kufanya mapitio na sera Sheria za uvuvi pamoja na kuimarisha taasisi zake ili kuweza kuongeza ushiriki katika uchumi wa buluu pamoja na kuwajengea uwezo wavuvi kufanya shughuli zao katika bahari kuu.
Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa mradi kutoka shirika la Mwambao Mkoani Tanga Kengela Mashimba alisema kuwa ili kuweza kuinufaisha jamii kupitia mazao ya bahari Kuna haja ya kuhakikisha ustawi wa bahari unakuwepo wakati wote huku akiiomba Serikali kuwapa elimu na uwezo wa kuweza kufanya doria sambamba na urejeshaji wa mikoko na matumbawe ili waendelee kunufaika na mazo yatokanayo na bahari.
"Mwambao tunaamini kwamba ustawi wa bahari ni utajiri wa jamii, hatuwezi tukawa na ustawi wa bahari pasipo na jamii kushiriki moja kwa moja katika kuzisimamia rasilimali zilizopo kwa kuwajengea uwezo wa kuweza kusimamia rasilimali zake yenyewe itakuwa ni njia ambayo itaisaidia kuwa tajiri lazima wapewe elimu na kuwawezesha kufanya doria kufanya urejeshaji wa mikoko na matumbawe" alisema Mashimba.
Post A Comment: