Afisa Tarafa wa Tarafa hiyo Mapesah Makala akiwa eneo la chanzo cha maji katika tarafa hiyo.


Na Fredy Mgunda, Iringa.

Wananchi wa Tarafa ya Idodi wilaya ya Iringa mkoani Iringa wametakiwa kuendelea kuvitunza na kuvilinda vyanzo vya maji kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na msumba news,Afisa Tarafa wa Tarafa hiyo Mapesah Makala alisema kila Idara na Serikali za vijiji ni vyema kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi juu ya Umuhimu wa kutunza utajiri wa vyanzo vya  Maji na matumizi sahihi ya Maji ili kulinda Maji kwa sasa na baadaye

Makala alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inampango wa kujenga bwawa kubwa kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Tarafa hiyo chini ya Wizara ya Maji ikiongozwa na Mh Waziri Aweso

Na ikumbukwe wazo hili liliibuliwa na Mbunge wa jimbo la Ismani William Lukuvi katika kuhakikisha Idodi inakuwa na Maji ya uhakika zaidi hapo baadaye

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: