Na Denis Chambi, Tanga.

WAKALA wa Misitu Tanzania 'TFS' umepata somo katika michuano ya 'SHIMUTA' kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa michezo hiyo kwa watumishi wa Umma hapa nchini umefanikiwa kufika fainali kwenye mchezo wa mpira wa mguu hatua ambayo imewapa nguvu na kuona kuna haja ya kuanza kuwekeza zaidi katika sekta ya michezo.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkoani Tanga mara baada ya kutamatika kwa michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la michezo ya mashirika ya umma, taasisi na makampuni binafsi 'SHIMUTA' Kamishina msaidizi mwandamizi kutoka wakala Misitu Tanzania 'TFS' Erasto Luoga amesema kuwa kwa mwaka 2024 wamefanikiwa Kwa asilimia 90 kutimiza malengo yao licha ya uchanga walionao kwenyeichezo hiyo lakini wamefanikiwa kuziacha taasisi na makampuni na mashirika konge ambayo wamekuwa ni wazoefu.

"Hatukutegemea sana kama tutafika hatua hii kwa sababu ndio tunaanza tulichojifunza ni kuona kwamba kumbe inawezekana , tunakwenda sasa kuongeza nguvu ili mashindano yajayo tufanye vizuri zaidi"

"Sasa tunafanya maandalizi ya utengenezaji wa viwanja kwenye maeneo ambayo tutakuwa tunafanyia michezo kwenye maeneo yote ya taasisi kanda zote Saba tutahakikiaha kwamba kuna viwanja vya mpira wa mguu, mpira wa Pete, Kikapu na michezo mingine ili kuhakikisha kwamba watumishi wanashiriki michezo hiyo na tuweze kutengeneza timu bora" alisema Kamishna Luoga.

Kwa upande wake Mratibu wa michezo kutoka wakala wa Misitu Tanzania 'TFS' Maliseli Bitulo ameeleza kuwa kwa jinsi ya uchanga wao katika michezo hiyo kufika fainali ni jambo la kujipongeza hususani kwa wachezaji ambao waliipambania timu mpaka kufika fainali ambao wamewezesha malengo yao kutimia kwa zaidi ya asilimia 90.

Aidha Bitulo meupongeza na kuushukuru uongozi Mamlaka ya Misitu Tanzania 'TFS' kwa maandalizi ya timu ambao wamewezesha kufika fainali huku akipeleka ombi kupewa muda wa kutosha wachezaji wa timu kuweza kujiandaa ili kushiriki vyema katika michuano inayofanyika kila mwaka hapa nchini.

"Tumepita mechi nyingi mpaka kufika fainali haikuwa rahisi kupambana na timu 64 mpaka kufika hapa tumejtahidi sana tunawapongeza wachezaji wetu malengo yetu yametimia kwa asilimia 90 tutapeleka ombi letu kwa mamlaka tupate muda mzuri na wa kutosha kwaajili ya kuziandaa timu baada ya mashindano ya bonanza letu la mwaka tupate angalau wiki mbili za kukaa pamoja ili kutengeneza muunganiko mzuri kwenye timu"

"Ni mara yetu ya pili kushiriki michezo hii kwa uchanga wetu tunajipanga tena mwakani tuone tutafanya nini, nitawashauri baada ya mashindano yetu ya bonanza angalau tuwe na muda mzuri walau hata wiki mbili au zaidi za kuwa pamoja ili tuweze kuijenga timu kwenye muunganiko " alisema Bitulo

TFS ilipoteza mchezo mbele ya timu ya mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' baada ya kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara tatu katika kipindi cha kwanza katika fainali ya iliyochezwa Mkoani Tanga za kumtafuta bingwa wa michuano hiyo kwenye mpira wa miguu kwa mwaka 2024.

Mbali na mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano ya SHIMUTA kwa mwaka 2024 wakala wa Misitu Tanzania 'TFS' imeshiriki pia katika michezo ya Darts , Draft na Karata ambapo wamefanikiwa kutwaa medal mbili.


Share To:

Post A Comment: