Waziri wa Maliasili na Utali,Balozi Dkt Pindi Chana amemwagiza Kamishina wa Wakala wa Huduma na Misitu{TFS},Professa Do Santos Silayo kuhakikisha idara hiyo inakujikita katika kukusanya mapato katika mfumo TEHAMA lengo ni kutaka idara hiyo kukusanya zaidi mapato ya serikali.

Balozi Chana alisema hayo Jijini Arusha wakati akifungua Mkutano Mkuu wa tatu wa Makamanda wa TFS Nchini na kusema kuwa malengo waliyovuka ya kukusnaya mapato ya shilingi Bilioni 166 sawa na asilimia 103 kama wangekuwa wanatumia mfumo wa TEHAMA malengo hayo yangekuwa makubwa zaidi kuliko ilivyo sasa.

Alisema wakati umefika kwa TFS kukusanya mapato kwa mfumo wa TEHAMA kwani idara nyingi za serikali zimejikita katika mfumo huo lengo ni kuwa mfumo huo unakuwa salama na hauwezi kuchezewa na fedha za serikali zinakuwa salama.

''Ninakuomba Kamishina sasa mnapaswa kubadilika na kukusanya mapato kwa mfumo wa TEHAMA ili mapato yawe mengi na salama na malengo yaliyokusdiwa yazidi kupaa kwa asilimia zaidi ya mia moja''alisema Balozi Chana 

Akizungumzia uadilifu katika Kazi,Balozi Dkt Chana aliwataka Makamanda wa TFS kufanya kazi kama Makanda wa Jeshi kama walivyo baada ya kutoa katika mfumo wa uendeshaji Kiraia ikiwa ni pamoja na kuwa wazalendo katika kazi.

Balozi Dkt Chana Alisema sifa kuu ya askari kwanza ni kuwa mzalendo,muadilifu na muaminifu hivyo Makamanda wa TFS wanapaswa kwenda sambamba na misingi hiyo ili kulinda misngi ya kazi katika uendeshaji kazi za kila siku.

Alisema TFS inapaswa kufanya kazi kisasa ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kununuwa vitendea kazi vya kisasa ikiwa ni pamoja na magari ya kisasa,ndege na helkopta vyote vinahitajika katika utendaji kati katika misitu.

Waziri huyo alisema kuwa pamoja na hayo ameitaka menejimenti na Bodi ya TFS kuhakikisha wanatatua changamoto za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawapandisha vyeo wanapostahili na kuongezewa maslahi kwa wakati.

Alisema watumishi wa TFS wakiangalia kwa jicho la tatu katika maslahi shughuli za utendaji kazi za kila siku za Taasisi hiyo zitazidi kusionga mbele na makusanyo ya mapato ya serikali yatakuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka kwa kuwa wafanyakazi wanatatuliwa changamoto zao.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TFS, Brigedia Jeneral Mbaraka Naziad Mkeremy alisema kuwa TFS imejipanga kuhakikisha malengo ya makusanyo ya kila mwaka yanafikiwa na kuzidi ili taasisi hiyo iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa BodiMhandisi Enock Nyanda ambaye ni mjumbe wa Bodi ya TFS alisema kuwa Bodi kwa kushirikiana na menejimenti imekuwa ikishirikiana katika kuhakikisha inajali maslahi ya wafanyakazi na kutatua changamoto zinazowakabili.












    
Share To:

Post A Comment: