Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu ,Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuripoti Habari kuhusu uchaguzi huo Kwa kuzingatia haki, maadili,weledi, taratibu na Sheria zinazopaswa kufuatwa na si kutoa habari ambazo zita sababisha taharuki.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya habari maelezo Zamaradi Kawawa wakati akifunguua mafunzo Kwa waandishi wa  Habari kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi  Mkuu wa mwaka 2025 yaliyoandaliwa na Mtandao wa Mashirika yanayotoa Huduma za Msaada wa Kisheria Tanlap.

Mafunzo hayo  ya Siku mbili yamehudhuriwa na  waandishi wa habari zaidi ya 100 kutoka vyombo vya habari kutoka mikoa tofauti  nchini Tanzania.





















Share To:

Post A Comment: