Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeona kwa jicho la mbali, fursa kwa Watanzania wazawa katika kuendesha makampuni makubwa itakayowawezesha kuingia kwenye Soko la ushindani la Hisa na kuchukua kazi za miradi mikubwa, ambayo kwa asilimia kubwa inaendeshwa na Makampuni ya kigeni kutoka nje.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo, amewashauri Wamiliki wa Matipa na Mitambo nchini (TTMOA), kuanzisha Kampuni kubwa Kandarasi, yenye misingi ya kiuchumi ambayo itaweza kuwekwa kwenye Soko la Hisa na kufanya kuwa kampuni kubwa zaidi ambayo itaweza kuchukua kazi za Miradi mikubwa nchini.
Ni wakati sasa kwa Watanzania wazawa wanaomiliki Matipa na Mitambo, kuamka na kuchangamkia fursa hiyo kutokana kuwepo kwa changamoto ya wageni kutoka nje ya nchi, kufanya shughuli ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya.
Katika kuwashauri Wamiki hao, Waziri Jafo amesema, endapo umoja huo utaweza kuanzisha kampuni hizo kubwa, basi utaweza kuwa na nafasi kubwa kama wazawa kupewa miradi mbalimbali.
Katika kufunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama Wamiliki wa Matipa na Mitambo (TTMOA) Jijini Dar es Salaam, Waziri Dkt.Jafo, amewaahidi wamiliki hao kuwa, atashirikiana na Wizara za Kisekta kutatua changamoto zao, ikiwemo kupewa miradi ambayo wazawa wanaweza kuifanya, kwani kumekuwa na changamoto ya wageni kufanya shughuli ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya, pia ili kuwafanya Watanzania kuwa na uchumi ili kuendana na dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amewataka Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa endapo wanaandaa michakato ya kutoa maeneo ya kuchimba vifusi na madini ujenzi mengine, wawaangalie Watanzania kwanza, kwani Sekta hiyo inawagusa Watanzania moja kwa moja na inatoa kiasi kikubwa cha ajira kwa Watanzania.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Emmanuel Moshi, ameishukuru Serikali kwa kuona haja ya kulinda wazawa na wafanyabiashara wa ndani ili kuwa sehemu ya ujenzi wa miradi na kuwezeshwa kwenye uwekezaji wa miradi.
#KAZIINAONGEA
Post A Comment: