Kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Sekta ya Madini Tanzania 2024

•Dhima: "Kuongezea Thamani Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii."

Malengo ya Mkutano:

•Kutangaza fursa zilizopo katika sekta ya madini.

•Kubadilishana uzoefu na kukuza uwekezaji.

•Kujadili teknolojia za kisasa za uchimbaji na usafishaji madini.

•Kuhakikisha madini yanachangia katika uchumi kwa kuongezewa thamani.

Nafasi ya Tanzania Katika Sekta ya Madini

•Tanzania inaendelea na mkakati wa kuwa kitovu cha madini barani Afrika.

•Nchi nyingine zinajifunza kutoka Tanzania kuhusu usimamizi bora wa sekta ya madini mfano mzuri ni majirani zetu Malawi. 

•Utafiti wa kina wa madini umeimarishwa, nanSerikali imewekeza zaidi katika miundombinu ya sekta.

Mnyororo wa Sekta ya Madini:

•Kuanzia utafiti, uchimbaji, usafishaji, biashara, na utoaji wa huduma migodini.

Madini Mkakati:

•Tumejaaliwa kuwa na aina nyingi za madini muhimu yanayohitajika kwa ajili ya nishati safi kama vile nikeli, kobalti, kinywe, gesi ya Helium na mengine. 

•Madini muhimu kwa nishati safi ni nyenzo za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

•Madini haya yanachangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi huku yakilinda mazingira.

•Mwekezaji yeyote anayekuja kuwekeza nchini lazima atuonyeshe mpango wa kuyasafisha au kuyaongezea thamani hapa hapa nchini madini muhimu. 

Uwezeshaji:

•Tozo zimepunguzwa kutoka zaidi ya 30% hadi 9.3%.

•Wachimbaji wa dhahabu wanaotumia refineries za ndani wamepewa msamaha maalum wa kodi.

•Benki Kuu ya Tanzania sasa inanunua dhahabu ili kuimarisha akiba ya fedha za kigeni.

Mfumo wa Masoko:

•Masoko 43 na vituo vya ununuzi wa madini 105 yameanzishwa ili kuhakikisha wachimbaji wanapata uhakika wa soko na bei elekezi.

•Mfumo huu pia unasaidia kudhibiti utoroshaji wa madini na kuimarisha mapato ya serikali.

Programu ya Mining for Brighter Tomorrow (MBT) inalenga vijana na wanawake kwa kuwapatia:

•Vifaa vya uchimbaji ili wafanye shughuli zao kwa tija zaidi.

•Kuwapatia Leseni za uchimbaji ili wafanye shughuli zao bila usumbufu. 

•Elimu kuhusu teknolojia na upatikanaji wa mikopo nafuu kupitia Taasisi za fedha na mabenki kwa uratibu wa serikali.

•Serikali kupitia STAMICO imeagiza mitambo ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo, mitano ilishawasili na kukabidhiwa wachimbaji wadogo na mengine 10 itawasili hivi karibuni.

•Msaada wa vifaa maalum, kama magari kwa kina mama.

Mafanikio na Malengo ya Sekta

•Sekta ya madini inachangia 9% ya Pato la Taifa (GDP), huku lengo likiwa kufikia 10% mwaka 2025.

•Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika kurasimisha sekta ya uchimbaji mdogo, jambo linalosaidia kukuza ajira na uchumi wa jamii.

Ushirikiano wa Sekta ya Madini na Jamii

•Uchimbaji Mkubwa:

•Kampuni kubwa zinatekeleza wajibu wa kijamii (CSR) kwa jamii zinazozunguka miradi yao kama vile ujenzi wa miradi kwa ajili ya huduma za kijamii, barabara, maji na kadhalika.

Utekelezaji wa Ushiriki wa Watanzania:

•Mkazo umewekwa katika local content, kuhakikisha Watanzania wanashiriki moja kwa moja katika sekta ya madini kupitia ajira, huduma, na biashara.

•Hii ni sehemu ya jitihada za serikali kuifanya sekta ya madini kuwa kichocheo kikuu cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watanzania wote.

Share To:

Post A Comment: