Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, leo November 12 2024, amefanya mazungumzo na Balozi wa Ireland  Mhe. Nicola Brennan

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha uhusiano kati ya Arusha na Ireland , na pia kujadili fursa za ushirikiano katika sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya Utalii, Elimu na kadhalika.

Mhe. Makonda alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika mkoa huo huku Balozi huyo akiahidi kuendeleza mashirikiano kati ya Serikali ya Ireland 🇮🇪 na Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Share To:

Post A Comment: