Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dk Batilda Burian amaeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa maandalizi mazuri ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Mhe Balozi Dk Batilda Burian ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Handeni  katika muendelezo wa ufuatiliaji wa maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Aidha amewataka wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo, ili uchaguzi huo wa Novemba 27, 2024 uwe wa huru na haki  pasipo na shaka yoyote.

‘’Ni dhamira na utashi wa kisiasa wa Mhe Rais Dk Samia Suluhu Hassan, kuona uchaguzi huo unatoa fursa pana kwa kila raia, kutumia haki yake ya kikatiba kugombea, ama kumchagua kiongozi anayemtaka’’ Mhe Balozi Dkt. Batilda amesema.












Share To:

Post A Comment: