Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili mjini Havana, nchini Cuba linalotarajia kuanza Novemba 7 hadi 10, 2024
Rais Dkt Samia ataungana na Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, kuhudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara zinazohusika na utamaduni kutoka Tanzania na Cuba kuandaa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili.
Takriban watu 600 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo ambao ni pamoja na mawaziri, wawakilishi kutoka sekta binafsi, mashirika yanayoangazia lugha ya Kiswahili na vyuo vikuu kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Aidha kongamano hilo litahusisha semina mbalimbali na uzinduzi wa kamusi ya Kiswahili ya Kihispania iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kiswahili kimepata maendeleo makubwa baada ya kutambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuwa lugha ya saba ya kimataifa, ikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 500 duniani kote.
Post A Comment: