Na Denis Chambi, Tanga.

JAJI Mkuu wa Mahakama  ya Tanzania Prof. Ibrahim Juma amevitaka vyuo vinavyofundisha kada ya Sheria hapa nchini kuendana na kasi ya  maendeleo ya kidigital ili kuweza kuwaandaa wanafunzi  wa taaluma hiyo  kuja kupambana na soko la ajira sambamba na kulisaidia Taifa kuweza kuwa watendaji wenye umahili katika kazi.

Professional Juma ametoa Rai hiyo Mkoani Tanga wakati wa Mahafali ya 24 ya chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto 'IJA' yaliyofanyika November 29  ambapo amesema kuwa bado vyuo vinavyotoa elimu hiyo hapa nchini mitaala yake ipo katika mfumo wa analogia hali ambayo haimjengi mwanafunzi kuendana na kasi ya maendeleo ya kisasa ambayo ipo kwenye Karne ya 21.

"Dunia ya sasa inaelekea katika mifumo ya kidigitali kwa bahati mbaya vyuo vinavyofundisha sheria hapa nchini bado mitaala yake ni ya kizamani haviwataarishi wanafunzi kupambana na changamoto  mtu yeyote ambaye anamaliza sheria eneo kubwa atakaloenda kufanya kazi ni mahakamani sasa kama Mahakama imeshaenda kwenye Karne ya 21 lakini vyuo bado vipo kwenye  ya 20 tunakuwa hatuwatendei haki wale wanafunzi" amesema Proffesa Juma.

Proffesa Juma amesisitiza mifumo hiyo ya kisasa kuanza Kufundishwa kwa watumishi wote  huku akiendelea kumsisitiza msajili wa Mahakama ya rufani  kuwapeleka nje ya nchi watunza kumbukumbu kwenda kujifunza namna mfumo mtandao unavyofanya kazi kwa urahisi badala ya kutumia makaratasi

Aidha katika kutatua changamoto hiyo iliyopo kwa sasa Proffesa Juma amesema kuwa tayari Mahakama imeshajiwekea lengo la kuhamia kwenda  kwenye mifumo ya kidigitali ambayo tayari wameshafunga mifumo ya Karne ya 21 akisisyiza wahadhiri vyuoni kuanza kuwafunssha wanafunzi ili kuwajengea uzoefu wanavali bado mashuleni

"Upo umuhimu kwa wahadhiri kuhamia katika ufundishaji wa kutumia mifumo ya kidigitali , Mahakama tumeshajuwekea lengo kwamba tutakuwa  ni  Mahakama mtandao ambapo shughuli zote za kiutawala na utoaji wa hali zitakuwa  kwa njia ya kidigitali tayari tumefunga mifumo ya Karne ya 21  sasa tutaomba wahadhiri tuhame  tuanze kuachana na makaratasi ili tuweze kuitumia mfumo huu ni lazima tuanze kuhama ili kuboresha itendaji kazi na kuleta ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi" amesisitiza Jaji huyo.

Proffesa Juma ameupongeza uongozi wa chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto  'IJA'  kwa jinsi walivyojipamabua kuendana na kasi ya Dunia ambapo wameweza kujenga jukwaa la kujifunzia, akiwataka kutumia uwezo walionao  kutoa elimu kwa wadau  mbalimbali wa Mahakama njia ambayo pia itaweza kuwaongezea mapato ya chuo.

Awali akizungumza mwenyekiti wa Baraza la chuo hiyo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya rufani Dkt. Mary Levira amesema kuwa  chuo kumekuwa kikitoa fursa ya kuwaendeleza kielimu watumishi wa mahakama hapa nchini huku akieleza mafanikio ya kiutendaji ambayo yamekofanya chuo hicho kuweza kutambulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania .

Ameongeza kuwa pamoja na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwa wadau ambayo yamewezeaha should kutambulika zaidi kimataifa bado wana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha kuwa  wanazidi kuboresha huduma wanazozitoa.

"Chuo kina mchango mkubwa katika uendelezaji wa watumishi  wa mahakama wa ngazi zote  kupitia mafunzo kwa kuwajengea uwezo ambapo Kwa kiasi kikubwa yamekuwa ni chachu ya maboresho yanayoendelea katika Mahakama ya Tanzania niipongeze menejimenti ya chuo kwa kazi kubwa wanaofanya ambayo imekifanya chuo kutambulika siku hadi siku ndani na nje ya Taifa letu kupitia huduma mbalimbali"

Mkuu wa chuo hicho ambaye ni Jaji wa Mahakama ya rufani Dkt Paulo Kihwelo amebainisha kuwa chuo kimeendelea kuimarisha mahusiano yake na wadau , taasisi za ndani na nje ya nchi pamoja  jamii kwa ujumla katika kutoa huduma ambapo wamefanikiwa kuwapatia elimu ya msaada wa kisheria na ushauri wananchi kuanzia ngazi ya 

"Katika kuhakikisha kuwa chuo kinafikia malengo yake na kuwa kimataifa  kimeendelea kuimarisha mahusiano yake na wadau wa ndani na nje ya nchi, kwa sasa chuo kina mahusiano na taasisi ya kimahakama ya Afrika na kufikia sasa tuna nchi 11 ambazo zina uwanachama katika mtandao huo lakini pia  tuna ushirikiano na shirika la kimataifa la kupambana na uhalifu pamoja na madawa ya kulevya"

"Chuo kimeweza kimeendelea kutoa msaada wa kisheria na ushauri binafsi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kutoa mafunzo kwa viongozi wa vijiji na vitongoji na kata mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Lushoto namna ya jinsi migogoro inavyotatuliwa" amesema Dkt. Kihwelo.

Hii ikiwa ni Mahafali ya 24  tangu kuanzishwa kwa chuo hicho  cha uongozi wa Mahakama Lushoto 'IJA' jumla ya wanafunzi 762  wamehitimu ambapo astashahada ya msingi ya Sheria wamehitimu wanafunzi 245, stashahada ya Sheria (279), na  astashahada ya Sheria 'Diploma in low ' 238.


Share To:

Post A Comment: