CHAMA cha National league for Democracy 'NLD' kimeitaka Ofisi ya Rais tawala za mika na Serikali za mitaa 'TAMISEMI' kupitia mapema taarifa za wanachama wake waliotia nia kuingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Serikali za mitaa kubaini kama Kuna mapungufu katika taarifa zao kabla ya November 8,2024 siku ambayo wagombea wote watapitishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Tanga katibu Mkuu wa NLD Taifa Doyo Hassan Doyo amesema kuwa wameridhishwa na mchakato wa uchaguzi tangu hatua za awali kufuatia kanuni zilizoundwa hali ambayo inaonyesha ukomavu wa kisiasa kutokana na vyama vyote kuwa tayari kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika 2024 ukifwatiwa na ule wa mwaka 2025 huku akiwataka wasimamizi wa uchaguzi kuwa waadilifu.
"Tunatoka wito kwa TAMISEMI kwamba tumerudisha fomu na tumefanya hivyo kwa mujibu wa kanuni na wanazo tangu tarehe 1 mpaka tarehe 8 ndio teuzi tunawaomba TAMISEMI kwa kuwa fomu wanazo muda mrefu kama kuna Mwana chama amekosea kujaza taarifa zake ni vyema wakawasiliana na wagombea mapema ili siku ya tarehe 8 wagombea wetu wote wateuliwe" alisisitiza .
Amesema NLD inaamini utashinda katika chaguzi za Serikali za mitaa zitakazofanyika November 27 hii ni kutokana na wanachama wake waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ambapo katika mikoa yote waliyoitemnelea Mkoa wa manyara umesika nafasi ya kwanza.
"Nchi nzima katika mikoa 10 ambayo tumesimamisha wagombea tuna mitaa hamsini maana yake chama chetu kimekubalika zaidi mjini lakini tuna vijiji 21 na vitongoji 40 hii ndio jumla ya wagombea kwa vijiji na Miata ambayo tumesimamisha wagombea" alisema Doyo.
Akizungumzia ziara yake aliyoifanya katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukiimarisha cha hicho kuanzia ngazi za mitaa vijiji na vitongoji Doyo alisema wamefanikiwa Kwa kiasi kikubwa ikiwa ni ishara njema kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika November 27,2024.
"Tulifanya ziara ya oparesheni maalumu katika mikoa 15 hapa nchini na ziara ambayo imetupa mafanikio makubwa kisiasakutokana na uchanga wa chama chetu, NLD Tutatumia kila kilichokuwa chetu kwa namna yeyote ile kuhakikisha kuwa NLD kinakuwa chama kikubwa na maarufa katika medani za siasa nchini Tanzania"
Aidha Doyo alisema chama hicho kinampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufwatia falsafa yake ya 4R ambazo zimeleta na kuchangia maelewano na ushirikiano kwa vyama vyote vya siasa hapa nchini hatua ambayo unakwenda kuleta maendeleo kwa Taifa.
"Tunamshukuru na kuipongeza sana TAMISEMI kwa kukubali na kupokea hoja za vyama vya siasa n kutusikiliza wadau wa siasa kuelekea uchaguzi wa mwaka huu hii ni ishara kuwa 4R za Rais Samia Suluhu Hassan zimefanya kazi mpaka vyama vya siasa vinaamini mchakato wa uchaguzi katika nchi yetu hii ni hatua kubwa sana katika nchi yetu"
2 Attachments • Scanned by Gmail
Post A Comment: