Na,Jusline Marco : Tanga.


Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA kupitia timu zilizopo katika mamlaka hiyo imewasili mkoani Tanga kushiriki katika Mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoanza leo tarehe 10 hadi 24 Novemba 2024, jijini Tanga. 

Kushiriki kwa NCAA kwenye mashindano hayo ya SHIMMUTA 2024 sio tu kunaleta ushindani, bali pia kunajenga mshikamano wa ndani na kuimarisha afya za wafanyakazi. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya NCAA,imesema Mashindano hayo yanatoa fursa kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete,riadha ikiwa ni sambamba na kuhamasisha utalii wa ndani kwa vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro

Taarifa hiyo imeongeza kuwa maashindano hayo yamejumuisha mashirika mbalimbali nchini yakiwa na lengo la kukuza mshikamano, afya, na ari ya ushindani miongoni mwa wafanyakazi wa mashirika hayo.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wa timu ya mchezo wa Kamba ya NCAA, Nelson  ameushukuru uongozi wa mamlaka kwa kuwapa msaada na motisha utaowawezesha kushiriki mashindano hayo kwa nguvu na hamasa kubwa wakiwa na ari mpya ya ushindi.

"Tumekuwa na maandalizi bora zaidi kuliko mwaka jana. Uongozi umetupa kila tunachohitaji ili tuweze kuwakilisha NCAA kwa heshima na nguvu," alisema Nelson

Naye Kapteni wa timu ya mpira wa pete ya NCAA, Halima Mbombe, amewahakikishia  mashabiki na wapenzi wa timu ya Ngorongoro kuwa, wamejipanga kurudi nyumbani wakiwa na vikombe.  

Hamis Mshana, mkufunzi wa timu ya mpira wa miguu ya NCAA, amesisitiza dhamira yao ya kurudi nyumbani na vikombe zaid na kuweka  wazi kuwa timu imekuwa ikifanya mazoezi makali na yenye malengo ya kupata ushindi wa hali ya juu.





Share To:

Post A Comment: