Na. Lusungu Helela

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amesema  Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni Taasisi nyeti kwa ajili ya  usalama  wa nchi kwani kwani hakuna Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) uliosanifiwa unaoweza kutumika nchini katika Wizara, Taasisi  au  Idara ya Serikali bila kuridhiwa na e-GA

 

Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akizungumza  na Wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala   Katiba na  Sheria katika kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa e-GA na Taasisi ya Uongozi  kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hizo ambapo amesema  tangu kuanzishwa kwake e-GA imeleta mageuzi makubwa huku akitaja mifumo mingi inayotumika kwa sasa Serikalini imebuniwa na   kusanifiwa na e-GA

 

Amesema ujio wa e-GA umeisaidia kupunguza gharama kubwa kwa  Serikali ukilinganisha na hapo awali ambapo  mifumo mingi iliyokuwa ikitumika kwenye Taasisi za Serikali ilikuwa ni ya kutoka nje huku akitolea mfano mfumo  wa manunuzi  wa TANEPS ulikuwa ukimlazimisha mtumiaji endapo kama anataka kufanya marekebisho ni lazima awasiliane na watengenezaji  wa mfumo huo ambao ni  Wagiriki

 

" Kama nchi kulikuwa hakuna usiri wa taarifa zetu, Wasanifishaji mifumo ya TEHAMA ambao ni wa kutoka Mataifa ya nje ndo walikuwa wenye ‘serve’ za taarifa zetu  amesisitiza Mhe.Sangu

 

Amesema  hapo awali Taasisi nyingi za Serikali zilikuwa zikitumia mifumo hiyo ya kutoka nje bila kuidhinishwa na e-GA ambapo ilikuwa  ni rahisi kuhujumu kwa lengo la kujinufaisha kwa kushirikiana na watu wa kutoka  nje ila kwa sasa hilo jambo haliwezekani kutokana na uwepo wa e-GA 

 

'" Upo ushahidi kabisa kwamba e-GA imesaidia kuboresha utendaji kazi, imeimarisha utawala bora, kupunguza vitendo vya rushwa ambavyo vingeweza kujitokeza, kuimarisha makusanyo na kudhibiti matumizi ya maduhuli ya serikali” Mhe. Sangu amesisitiza.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala,  Katiba na  Sheria  Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ameipongeza e-GA kwa kazi kubwa inayoendelea kuifanya huku akiitaka kjiimarisha zaidi kwenye eneo la ubunifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia yanayotokea dunia kote

 

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ameitaka e-GA kusanifu mifumo itakayosaidia kupunguza matatizo katika jamii ikiwemo upotevu mkubwa wa maji unaotokea  katika maeneo mbalimbali nchini.

Share To:

Post A Comment: