Na, Elizabeth Paulo; Dodoma
Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mh. Halima Okash ametoa Rai kwa Viongozi wa Halmashauri kusimamia sheria, kanuni na Taratibu za Kuongeza mapato ya Halmashauri kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato, kukusanya takwimu sahihi ,tathmini ya mara kwa mara na kuongeza usimamizi wa karibu kwa kila chanzo.
Akiongea katika kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 Mh.Okash amewataka Madiwani katika Kata zao kuongeza kasi ya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwa kushirikiana.
Hata hivyo Mhe. Okash Amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Chemba,ambapo amewakumbusha Waheshimiwa Madiwani hao kushiriki kwenye shughuli za maendeleo katika Kata zao, pamoja na kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa na ikamilike kwa Wakati.
Katika kikao hicho Baraza la Madiwani limeazimia kuunda kamati itakayotembelea shule zote zilizokua na ufaulu mdogo ili kugundua changamoto zinazoikubwa na kuzipatia ufumbuzi mapema.
Baraza Hilo linachukua azimio Hilo Mara baada ya Baraza la mtihani Tanzania (Necta) kutangaza matokeo ya Darasa la Saba , na kuonesha kuwa halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuendelea kuwa na ufaulu mdogo.
Post A Comment: