Semina ya Sheria za Uchaguzi na Vyama Vya Siasa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ushiriki wa Wanawake katika Siasa imefanyika Novemba 7 Mjini Bukoba ikiwa imeandaliwa na Mbunge wa Viti maalum kupitia makundi Maalum Neema Lugangira kwa Mabalozi wote wa CCM 227.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mabalozi hao wa CCM 227 katika semina hiyo Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) - Oganaizesheni Cde Issa Gavu, amejibu hoja zao na kutoa salaam za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Mabalozi wa CCM wa Bukoba Mjini.
Katika semina hiyo mada mbalimbali ziliwezeshwa na watoa mada akiwemo Katibu wa CCM Bukoba Mjini Shaban Mdoe sambamba na Katibu wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Bukoba Mjini Bi. Hadija Mkelenga kwa kuwasilisha Mada.
Semina hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano na Shirika la Omuka Hub na FES Tanzania.
Post A Comment: