Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed J. Gombati, ameongoza uzinduzi wa huduma maalum za kibingwa na ubingwa bobezi zinazohusiana na mifupa, ubongo, mgongo, na mishipa ya fahamu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) leo tarehe 6 Novemba 2024. Huduma hizi zitatolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya MOI ya Muhimbili.


Bw. Gombati amepongeza juhudi za hospitali kwa kufanya makubaliano ya ushirikiano na taasisi mbalimbali za afya, hatua ambayo itasaidia kupunguza gharama na usumbufu kwa wagonjwa waliokuwa wakienda Dar es Salaam kupata huduma hizi. Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa ya huduma hizi katika hospitali hiyo.



Dkt. Bryson Mcharo, aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa MOI, alieleza kuwa lengo ni kuleta huduma hizi karibu na wananchi wa kanda ya ziwa ili kupunguza matatizo ya kusafirisha wagonjwa mbali kwa matibabu. Sasa huduma za kibingwa za MOI zinapatikana moja kwa moja katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato.




Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: