Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kayombo, amesema madai ya CHADEMA ya mawakala wao kutoruhusiwa kuingia kwenye vituo hayana ukweli wowote kwa sababu mawakala wao wote walipewa barua zao za viapo. 

Kayombo amesema hayo Jijini Arusha baada ya Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, kudai kuwa vituo vingi vya kupigia kura mawakala wao wamezuiliwa kuingia kwenye vituo amesema siyo kweli na kwamba vituo vyote vimefunguliwa saa 2:00 asubuhi mawakala wa vyama vyote vyenye viapo wakiwepo. 

Kwa mujibu wa Kayombo hakuna malalamiko yoyote waliyoyapokea kutoka CHADEMA au chama chochote cha siasa na uchaguzi unaendelea vizuri.

Share To:

Post A Comment: