Makusanyo na Mafanikio ya Sekta ya Madini
Mwaka wa Fedha 2015/16: Sekta ya Madini ilikusanya shilingi bilioni 161.
Mwaka wa Fedha 2023/24: Makusanyo yaliongezeka hadi bilioni 753.
Mwaka wa Fedha 2024/25: Lengo la makusanyo ni trilioni 1, ambapo katika robo ya kwanza pekee zimepatikana zaidi ya milioni 300.
Mafanikio haya yanatokana na Mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017, ambayo yameimarisha ufuatiliaji na uwazi katika sekta.
Uanzishwaji wa Masoko na Vituo vya Ununuzi
Masoko 43 na vituo vya ununuzi 105 vimeanzishwa kudhibiti utoroshaji wa madini na kuongeza uwazi katika biashara.
Hatua hiyo imesaidia kudhibiti utoroshaji wa madini lakini kwa wale wachache waliokamatwa wakitorosha madini na kupatikana na mahakama kuwakuta na hatia, Serikali imechukua hatua kali ikiwemo kufuta leseni zao na hawaruhusiwi kufanya biashara ya madini tena hapa nchini.
Mazingira Bora kwa Wachimbaji Wadogo
Mmnamo mwaka 2019: Wachimbaji walikuwa wakilipa zaidi ya asilimia 30.3 ya mapato yao kama kodi na tozo lakini baada ya Serikali kusikiliza changamoto zao, hivisasa, Serikali imepunguza tozo na kodi hadi asilimia 9.3, na wachimbaji wanaopeleka dhahabu kwenye mitambo ya kusafisha hawalipi mrabaha, hivyo wanabakiwa na asilimia 4 tu.
Serikali imekuwa ikiwekeza kwa kuwasaidia wachimbaji wadogo, ikiwemo manunuzi ya mitambo ya uchorongaji kupitia STAMICO ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija.
Pia, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanzisha program maalum ya Mining for Brighter Tomorrow (MBT) kwa lengo kusaidia vijana na wanawake kujihusisha katika uchimbaji wenye manufaa.
Kuhusu Madini ya Almasi na Tanzanite
Almasi: Mahitaji duniani yameshuka kutokana na ongezeko la almasi za maabara.
Tanzanite: Serikali imerejesha hadhi ya madini haya kwa kutunga sheria na kurudisha masoko ya ndani. Sheria mpya inaruhusu minada ya ndani na ya kimataifa ya madini ya vito.
Maudhui ya Ndani (local Content) na Ajira kwa Wazawa
Ajira za moja kwa moja kwa Watanzania katika sekta ya madini zimefikia zaidi ya 16,000, huku nafasi za juu kwa baadi ya miradi mikubwa zikiwa mikononi mwa watanzania wazawa.
Kampuni za Kitanzania zinashiriki moja kwa moja katika kusambaza bidhaa na huduma kwa migodi Mikubwa hali inayopelekea kunongeza ajira kwa Watanzania na mzunguko wa fedha kubaki hapa nchini.
Madini Mkakati na Muhimu kwa Teknolojia ya Kisasa
Tanzania ina madini muhimu yanayotumika katika teknolojia za hali ya juu na viwanda:
Kinywe (Graphite): Muhimu katika utengenezaji wa betri, hasa kwa magari ya umeme.
Nikeli: Hutumika katika chuma kisichoshika kutu na betri za lithiamu-ioni.
Kobalti: Hutumika kwa betri na uhifadhi wa nishati.
Lithiamu: Muhimu kwa betri za magari ya umeme.
Madini Adimu ya Ardhi (Rare Earth Elements REEs): Kama niobium na tantalum, yanayotumika katika simu, mitambo ya upepo, na vifaa vya kijeshi.
Mkakati wa Kuongezea Thamani Madini Nchini
Malengo ya 2050: Dunia inapanga kuachana na magari ya petrol na dizeli. Tanzania imejikita katika kuongeza thamani ya madini hapa nchini badala ya kuyasafirisha ghafi, ili kuboresha ajira na uchumi.
Kiwanda cha Kusafisha Makinikia: Hekari zaidi ya 1300 zimetengwa Buzwagi kwa ajili ya kiwanda cha kusafisha madini, ambako Nikeli kutoka Kabanga Nickel itasafishwa.
Leseni ya uchimbaji haitatolewa kwa wawekezaji ambao hawajawasilisha mpango wa kujenga kiwanda cha kusafisha madini hapa nchini, kwa mujibu wa sheria ili kulinda ajira za watanzania.
Gesi ya Helium na Fursa kwa Madini ya Kinywe
Tanzania ina hifadhi kubwa ya gesi ya Helium katika Songwe na Rukwa, inayotumika katika vifaa vya matibabu kama MRI.
Tanzania ni ya tatu Afrika kwa uzalishaji wa Kinywe (Graphite), na mradi mkubwa unatarajiwa kuongeza uzalishaji ili kuimarisha nafasi ya nchi katika sekta hii duniani kote.
Kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini 2024
Tarehe: Novemba 19-21, 2024.
Mahali: Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mkutano huu unaleta pamoja wawekezaji, viongozi na wawaziri wa kisekta kutoka nchi mbalimbali, na maafisa kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kukuza uwekezaji katika sekta ya madini.
Kipekee, tunamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini, mfano kampuni ya BHP inatarajiwa kurudi kuwekeza nchini kupitia mradi wa Kabanga Nickel baada ya kusitisha shughuli zake barani Afrika zaidi ya miaka 15 iliyopita.
Post A Comment: