Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Aretas Lyimo, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Mamlaka hiyo, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Bw. Andambike Mololo wa Wizara hiyo, Kamishna wa Utawala DCEA, Shaaban Khatib Baraza na Kamishna Msaidizi Mipango na Bajeti DCEA, Lusajo Gilbert .
Post A Comment: