Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ametoa wito kwa Wabunifu na Wakadiriaji majenzi nchini kuwa Wazalendo, Waadilifu na Wabunifu kwa Taifa katika Utekelezaji wa Taaluma zao nchini.
Mpogolo ametoa wito huo Mkoani Dar es salaam alipomuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Nishati Doto Biteko na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila katika Mkutano Mkuu wa Tano wa Bodi ya usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ( AQRB) na kuwataka kutumia Teknolojia ya Kisasa na rahisi ili kuendana na wakati na kupunguza gharama za Ujenzi.
Mpogolo amesema, " Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa na inatoa fedha nyingi sana kwenye miradi mikubwa ya kimkakati na ya huduma za jamii hivyo inategemea na uadilifu wetu, utaalamu wetu na umoja wetu ili kushindana na wataalamu toka nje."
Aidha Mpogolo amewahimiza wataalamu hao kutumia teknologia bora na rahisi ili kuongeza Ubora wa Ujenzi na Muda wa Utekelezaji wa Miradi wanayopewa na serikali kwa kuwa wao ndiyo wabunifu wa michoro na wakadiriaji wa mahitaji na thamani halisi ya miradi.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ameipongeza Bodi na Wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB) kazi kubwa Walioifanya na kuifanya Tanzania inabadilika kila kukicha. Aidha ameipongeza Bodi kwa kuwasajili wataaluma 1586 kati yao wageni 33 tu, na kusajili Makampuni 473 kati ya hayo ya kigeni 6 tu na Wataalamu zaidi ya 8600 wamepewa mafunzo ya kuimarisha ujuzi wao kupitia mikutano yao mikuu.
Aliyosema " haya ni mapinduzi makubwa ya maendeleo yaliyofanywa Bodi ya AQRB chini ya Mwenyekiti Dkt. Ludigija Bulamile na timu yako ya kuongeza wajuzi wenye weledi wa kazi za Ubunifu na ukadiriaji majenzi"
Mpogolo ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wabunifu hao kuunga Mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo miradi mikubwa imetekelezwa kwenye nyanja za Miundombinu ya Barabara na Madaraja makubwa, treni ya Kisasa, Miradi ya Umeme, miradi ya Maji, Ujenzi wa majengo makubwa ya Serikali na watu binafsi, Ujenzi Mashule na Vituo vya Afya nchini.
Mpogolo amewata kuwa wamoja, wapendane na kushirikiana ili kushindana na Wataalamu wa Nje kutekeleza Miradi mikubwa ambayo inahitaji ujuzi mkubwa na mtaji mkubwa.
Ameongeza kuwa Mheshimiwa Rais Samia ameendelea kusimamia Sera ya Manunuzi ya Mwaka 2024 ya kulinda wataalamu wa ndani kwanza kwenye manunuzi (local content) na kuwapa kipaombele.
Aidha katika Mkutano huo Mkuu wa tano Mpogolo amepokea changamoto za kutaka halmashauri zote nchini kuajiri wataalamu hao wa ubunifu na usanifu wa majenzi, na uwepo wa sheria Mama kwa Nchi nzima itakayokuwa inasimamia masuala yote ya ubunifu na ukadiriaji majenzi.
Post A Comment: