Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ameongoza maadhimisho ya Siku ya Lishe Duniani, ambayo kiwilaya yamefantika  katika viwanja vya Shule ya Msingi Majohe, huku akitoa maelekezo kadhaa.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, jijini Dar es Salaam,  DC Mpogolo, ameelekeza  chakula  kutolewa shuleni kuwa ni jambo lazima hivyo kuzitaka kamati za shule, maofisa elimu kata na watendaji kusimamia utekelezaji.

Amesema, wakuu wa shule kamati  za shule na maofisa elimu kuweka mikakati bora ya matumizi ya chakula shuleni.

Ametaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wataalamu wa afya na lishe kuongeza elimi ya lishe hususan  kuwepo siku maalumu ya  lishe shuleni.

“ Angalau kila baada ya miezi mitatu shule iwe sekondari au msingi wanafunzi washiriki siku ya lishe. Wajue namna ya kuandaa lishe bora,”ameeleza DC Mpogolo.

Mkuu huyo wa Wilaya pia amesisitiza auanzishwaji wa klabu za lishe shuleni.

Ameeleza klabu hizo zitasaidia  kutoa elimu ya lishe na kusimamia maadili.

DC Mpogolo, pia aliwataka wanaume kuhakikisha wanaacha fedha ya kutosha ya matumizi katika familia zao na kuepuka matumizi makubwa katika masuala ya starehe.

Ameeleza, wapo wanaume ambao huacha fedha zisizotosheleza familia kula mlo kamili   hivyo kufanya watoto kukosa lishe bora.

“Wanaume wenzangu tuache tabia hiyo. Unamwachia mama sh.2000. Anajiuliza mama namna ya kuweka mambo sawa mpaka haelewi. Lakini wapo wanatumia fedha nyingi kunywa bia na starehe,”DC Mpogolo.

Mpogolo, ameitaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kuwapa motisha watoa huduma za lishe wa kujitolea kwani wanafanya kazi kubwa ya uhamasishaji.

Alisema licha ya kujitolea halmashauri inaweza kuwapa motisha kwa chochote kinachopatikana katika kampeni za lishe hali itakayo watia moyo wa kufanya vizuri zaidi.

Amesema, afya ni jambo muhimu  na msingi wake ni lishe bora  ambayo huchangia hata katika nguvu kazi ya taifs

Amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya pamoja na kuwa kinara wa lishe.

Awali Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk. Hamza, amesema jiji  hilo limepunguzs udumavu kutoka asilimia 03 hadi 01.

Amemshukuru Rais Dk. Samia kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya na kueleza rais amejidhihirisha wazi kuwa kweli ji Daktari halisi wa falsafa. 








Share To:

Post A Comment: