Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea wamejitokeza kushiriki katika zoezi la upigaji kura linalofanyika Leo November 27 2024 katika vituo vyao walivyojiandikisha.
Awali mkuu wa wilaya hiyo Mhe Mohammed Moyo ameshiriki zoezi Hilo katika kitongoji chake cha Boma kata ya Boma mashariki na kueleza kuwa amejitokeza sehemu ambayo alijiandiksha na kusema kuwa utaratibu ni nzuri na kuwasihi wananchi kujitokeza kushiriki kwani kura Yako ni ya thamini katika miaka mitano ijayo.
Katika hatua nyingine Msimamizi wa uchaguzi wilaya Mhandisi Chionda Kawawa ameshiriki katika kitongoji cha Tulieni kilichopo katika kata ya Nangowe na kuwasihi wananchi kutumia haki zao za msingi Kwa kujitokeza kuchagua viongozi sahihi na kushukuru wadau wote walioshiriki katika kutoa elimi maeneo mbalimbali juu ya umuhimu wa uchaguzi huo na kueleza kuwa ni siku muhimu Kwa wilaya hiyo naTaifa kiujumla na kubainisha muda wa kazi katika vituo hivyo ni saa (2) mbili asubuh mpka saa 10 jioni.
Aidha nae Bw Ally Mkitage Ambae ni Msimamizi wa uchaguzi kata ya Nangowe amesema kata yake ina jumla ya vituo (15) Kuni na vitano na tayari vituo vyote vimeshakamilika na wananchi wameshajitokeza kupiga kura na kata ipo salama na matarajio yake mpaka kufikia saa (10) kumi wananchi wote watakuwa wameshapiga kura tayari
Katika hatua nyingine Bw Othumani Hassan Ambae ni mkazi wa kitongoji Cha Tulieni ameeleza kuwa yeye ameamasika kupiga kura Kwa maendeleo ya kitongoji chake na kuchagua viongozi Bora na kuwasihi wananchi wote waliojiandikisha kwenda kupiga kura na kuendelea na majukumu Yao ya kilasiku .
Post A Comment: