Na, Jusline Marco : Arumeru,Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Amir Mkalipa amewataka wajasiriamali Wilayani humo kutumia mikopo ya asilimia 10 kujiendeleza kibiashara na kuepukana na mikopo ya kausha damu yenye riba inayoumiza.
Akigawa vitambulisho 929 kwa wajasiriamali wanaojishughulisha na uuzaji wa bidhaa mbalimbali ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawaji wa vitambulisho hivyo kati ya wajasiriamali 1501 sawa na asilimia 75 ya wajasiriamali waliojiandikisha na kusajiliwa.
Amesema upokeaji wa vitambulisho hivyo ni kutimiza haki na wajibu ambapo ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuvuka lengo katika ukusanyaji wa mapato yake katika kota ya kwanza.
Mkalipa amesema kazi ya Serikali ni kuhakikisha ustawi wa biadhara za wajasiriamali unaendelea kupitia vikundi vilivyopo katika kata husika ambavyo hupatiwa mikopo ya asilimia 10.
Awali akizungumza katika Mkutano wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Meru cha uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024 kwa mwaka wa fedha 2024/2025,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jeremia Kishili ameitaka idara ya usafi na mazingiria kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka eneo la dampo kujua madhara yanayotoka na uchomaji wa taka kabla ya halmadhauri kufanya jukumu hilo.
Kishili pia amewataka madiwani wa kata ya Maroroni na Uwiro pamoja na watendaji wa kata hizo kuhakikisha shule tarajali zilizopo kwenye kata zao zinafunguliwa kama ambavyo wananchi walitangaziwa na viongozi wa ngazi za juu ambapo pia ametaka amesisitiza elimu itolewa kwa wananchi juu ya mikopo na taratibu mpya zilizotolewa.
Akiwasilisha Kanuni mpya za utoaji na usimamizi wa Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashuri za mwaka 2025 pamoja na miongozo, Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa mikopo Bi.Regina Tilya amesema yapo baadhi ya maboresho yamefanyika kutoka kwenye kanuni iliyokuwa inatumika ya mwaka 2019 ambayo ni pamoja na umri kuongezwa kwa mkopaji hadi miaka 45, wanakikundi wanaokopa kufanya na kutekeleza mradi wa kila mwanakikundi.
Bi.Tilya maesema maboresho mengine ni kuwepo kwa kamati za huduma ya mikopo ngazi ya kata, halmashauri, na kamati ya uhakiki wa mikopo ngazi ya Wilaya,Ukomo wa mkopo na kima cha mkopo ambacho kimeainishwa kwenye muongozi na kanuni ambapo kikundi kinapata nafasi ya kukopa mara 3 huku kiadi cha juu vha mkopo kikiwa shilingi Milioni 150.
Post A Comment: