Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salum Hamduni (CP) ameshiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Msalala akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Mibako Mabubu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Rose Manumba.
Katibu Tawala Mh. Hamduni (CP) amelipongeza baraza la madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa ushirikiano mzuri walionao katika usimamizi wa miradi ya ujenzi iliyopelekea kukamilisha ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya na kuhakikisha viinaanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh.Mibako Mabubu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani kwa kurudisha mikopo ya asilimia 10 ambayo imekuwa ni chachu ya kukuza uchumi kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Pia Mh. Mabubu amepongeza hatua ya kuongezwa kwa umri wa ukopaji kwa vijana kutoka miaka 35 hadi miaka 45 ya ukopaji kwa vijana.
“Umri wa kuanzia miaka 18 hadi 35 vijana hao walikuwa wakisumbua hata katika urejeshaji wao, hivyo kuongezeka kwa umri wa vijana kukopa watapata nidhamu ya fedha wanayokopeshwa” amesema Mabubu.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mh. Mboni Mhita amewaomba madiwani wakawe mabalozi katika maeneo yao na kutoa elimu juu ya mikopo hiyo isiyo na riba ili kuepuka kutokea kwa dosari mbalimbali zitakazowafanya washindwe kurejesha kwa wakati mikopo hiyo ili iweze kuwanufaisha wengine.
Pia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Bi. Rose Robert Manumba amelishukuru baraza la madiwani pamoja na kamati zake kwa kuendelea kushirikiana vyema na watumishi sambamba na kutoa ushauri mzuri unaoijenga Halmashauri ya Msalala.
Kikao hicho kimehudhuriwa na waheshimiwa madiwani, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya msalala, wageni mbalimbali toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga pamoja na viongozi wa vyama rafiki vya siasa.
Post A Comment: