Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Charlotta Ozaki Macias Novemba 20, 2024 ametembelea Shule ya Msingi Muriet Darajani iliyopo jijini Arusha ambayo ina madarasa yaliyojengwa kwa ufadhili wa Mradi wa GPE (Global partinaship for Education).

Katika ziara hiyo Macias ameeleza kufurahishwa na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa ya Awali ya Mfano, matundu sita ya vyoo, tanki la maji,  na vifaa vya michezo ambao umegharimu zaidi ya sh. milioni 50.

Aidha Mhe. Balozi huyu pia  ameshuhudia ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa kupitia Mradi wa EP4R uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 100.

Balozi Charlotta Ozaki Macias ataendelea na ziara yake Mkoani Mara Kwa ajili ya  kukagua miradi ya elimu mingine iliyotekelezwa na GPE.












Share To:

Post A Comment: