Na Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, Mbeya
Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Wasimamzi wa Sekta ya Fedha nchini, imeandaa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa jijini Mbeya ili kuwawezesha wananchi kupata uelewa wa masuala ya fedha.
Maadhimisho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-nzovwe Jijini Mbeya yanalenga kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu matumizi ya huduma rasmi za fedha kwakuwa Serikali inakusudia takriban asilimia 80 ya wananchi watakuwa wamepata uelewa wa masuala ya fedha ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza alisema maadhimisho hayo pia yanalenga kuongeza mchango wa Sekta ya Fedha kwenye ukuaji wa uchumi.
Alisema kwa mujibu wa Utafiti wa FinScope wa mwaka 2023 nchini, ni asilimia 53.5 tu ya nguvu kazi ndiyo wanaotumia huduma rasmi za fedha na hivyo kubaki na kundi kubwa la Watanzania ambao hawafaidiki na huduma hizo.
“Kutotumia huduma rasmi za fedha kunasababisha wananchi kukosa fursa za kuboresha maisha yao kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi na hatimaye kuchangia katika kukuza Pato la Taifa”, alibainisha Bi. Hiza.
Alisema katika maadhimisho hayo wananchi watapatiwa elimu kuhusu faida ya kutumia huduma rasmi za fedha, usimamizi wa fedha binafsi katika utumiaji, uwekaji akiba pamoja na haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za fedha.
Bi. Hiza alisema kuwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi, pia watatoa elimu hiyo kwa wanafunzi ili waweze kujua umuhimu wa kutumia huduma za fedha wakiwa wadogo tofauti na ilivyo hivi sasa.
Alisema kuwa utamaduni huo ukijengwa katika ngazi hiyo ya chini uelewa unaweza kuwa mkubwa na faida kwa nchi kwani vijana wadogo wanaweza kutumia na kujua umuhimu wake wakiwa vijana.
Kwa upande wao Wasimamzi wa Sekta ya Fedha nchini kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji (CMSA), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) na Hifadhi ya Jamii wamewakaribisha wananchi kushiriki Maonesho hayo muhimu.’
Wamesema kutembelea maadhimisho hayo hawapati tu elimu bali na huduma zote zinazotolewa na taasisi hizo zinazopatikana katika Viwanja hivyo.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akizungumza katika mkkutano na wanahabari wa jiji la Mbeya, kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yatakayo fanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe, jijini Mbeya. Maadhimisho hayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa ya karibu.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania – TIRA, Bi. Hadija Maulid, akizungumza jambo wakati wa mkutano na wanahabari wa Jiji la Mbeya, ulioongozwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, (hayupo pichani), kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yatakayo fanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa ya karibu.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (Katikati), akizungumza katika mkutano na wanahabari wa Jiji la Mbeya, kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yatakayofanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa ya karibu. Wengine katika picha ni Meneja wa Idara ya Fedha na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bi. Maristella Kamuzora (wa kwanza Kulia), Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania – TIRA, Bi. Hadija Maulid (wapili kulia), Afisa Uhusiano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bi. Stella John (wa pili kushoto) na Afisa Mkuu wa Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul Njaidi (wa kwanza kushoto).
Afisa Mkuu wa Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul Njaidi, akizungumza jambo wakati wa mkutano na wanahabari waJiji la Mbeya, ulioongozwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (hayupo pichani), kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yatakayofanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe, jijini Mbeya, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa ya karibu.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (Katikati kulia), akiwa na baadhi ya Wasimamizi wa Sekta ya Fedha nchini, wakati wa Mkutano na wanahabari wa jiji la Mbeya, kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yatakayofanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe, Jijini Mbeya. Maadhimisho hayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa ya karibu.
Post A Comment: