Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe akizungumza na waumini na viongozi wa madhehebu mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) uliofanyika katika Kijiji cha Ikuyu

Baadhi ya Waumini wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe wakati akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) uliofanyika katika Kijiji cha Ikuyu
Diwani wa Kata ya Luhundwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe kwa ajili ya kuzungumza na waumini na viongozi wa madhehebu mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) uliofanyika katika Kijiji cha Ikuyu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe akiwa amewekewa mikono kichwani huku akiwa anaombewa na baadhi ya Wachungaji wa madhehebu mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania

Mwenyekiti wa Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu, Mchungaji Didas Mnyanyi akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe katika Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) uliofanyika katika Kijiji cha Ikuyu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe akiagana na baadhi ya waumini na viongozi wa madhehebu mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) uliofanyika katika Kijiji cha Ikuyu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe akisalimiana na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) uliofanyika katika Kijiji cha Ikuyu



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe amewataka waumini wa Kijiji cha Ikuyu kiichopo katika Tarafa ya Kibakwe Wilayani Mpwapwa kuwa mstari mbele katika kujitolea fedha na vitu mbalimbali ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoyakabili Makanisa badala ya kutegemea misaaada kutoka kwa viongozi.


Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waumini na viongozi wa madhehebu mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa Umoja wa Makanisa Ikuyu uliofanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT).


Amesema kipato cha wananchi wa Kijiji cha Ikuyu ni kikubwa kulingana na na shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazoziendesha ikiwemo kilimo cha kibiashara cha vitunguu na mahindi lakini majitoleo yao katika Kazi ya Mungu yamekuwa sio wa kuridhisha.


Amesema hali ya majengo ya Makanisa yaliyopo katika eneo hilo ni machakavu kutokana na waumini kutokuwa na utamaduni kwa kujitoa katika kazi ya Mungu.
 
‘’ Nimesilikiliza risala yenu mmeniomba nichangie zaidi ya Sh. Milioni 25 kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoyakabili makanisa yenu, nataka niwaambie ni lazima kila mmoja wetu ajitoe ili kufanikisha hili kwa pekee yangu nitachangia pale nitakapoweza’ amesema Mhe. Simbachawene.

Katika hatua nyingine, Mhe, Simbachawene amewaeleza waumini hao maendeleo yaliyofikiwa katika katika Kata ya Luhundwa ambapo shule za msingi nyingi zimejengwa ili kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.
 
Mbali ya shule pia zahanati imejengwa na kuwaondolea usumbufu wananchi kufuata huduma za afya kwa kutembea umbali mrefu.

Amesema Serikali inaendelea kuidhinisha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye Jimbo la Kibakwe na kwamba kata hiyo ni kati ya wanufaika wa miradi ikiwemo ujenzi wa shule, zahanati na sasa barabara ya Ikuyu imetengenezwa na inapitika wakati wote.

Mhe, Simbachawene ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Jimbo hilo huku akiwaomba viongozi hao wa dini kuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Rais Samia ili aendelee kuwatumikia Watanzania.
 
Kwa upande wake Mwenyekeiti wa Umoja wa Makanisa, Mchungaji Didas Mnyanyi amesema umoja wao umekuwa muhimu kwa ajili ya kuwahimiza wananchi Kutenda mem ana kuwa na sauti moja pindi jambo linapotokea la kuzungumza na wananchi amba oni waumini.

Umoja huo wa Makanisa ya Ikuyu umeundwa na Kanisa la Free la Pentecostal Church Of Tanzania (FPCT) Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT) Kanisa la Over Comers, Kanisa la Mitume na Kanisa la TAG.
Share To:

Post A Comment: