Waziri wa Madini,Mhe.Anthony Mavunde amevutiwa na ubunifu  wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wa kuwaweka wadau wake eneo moja kwenye  Maonesho ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Mhe.Waziri ametoa pongezi hizo leo tarehe 9 Oktoba wakati alipotembelea banda la STAMICO ambalo limepewa jina la "Kijiji cha STAMICO na Wadau Wake".

Alivutiwa  jinsi washiriki walivyojipanga kwa bidhaa mbalimbali kwenye sekta ya madini.

Pia alivutiwa na vikundi vya wanawake,watu wenye ualbino na watu wenye ulemavu wa usikivu ambao wanashiki kwenye maonesho haya kwa udhamini wa STAMICO.

Waziri aliambatana kwenye ziara hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhe.Martin Shigela pamoja na maofisa wengine kutoka serikalini.

Vikundi ambavyo vimealikwa na STAMICO na kushiriki ndani ya banda moja ni pamoja na FEMATA,TAWOMA, TAMAVITA,FDH,Tanzania Youth Miners na Chama cha Wachimbaji Geita (GEREMA).\n\nWengine ni pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia Geita na Chama cha Wanawake Geita (GEWOMA)

Waziri amepokelewa na Kaimu Meneja wa Masoko na Mahusiano wa STAMICO,Bw Gabriel Nderumaki ambae alimpatia maelezo mafupi kuhusu ushiriki wa Shirika kwenye maonesho haya mwaka huu.

Bw Nderumaki amesema kuwa STAMICO inajivunia kufanya kazi na vikundi mbalimbali vya wachimbaji na kuongeza  kuwa Shirika litaendelea kuvilea hivi vikundi.










Share To:

Post A Comment: