Na;Jusline Marco :Arusha
Waziri wa Afya nchini Jenista Mhagama amewataka wadau wa afya kuendelea kushirikiana na serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma za lishe ili kukabiliana na utapiamlowa aina zote nchini ambapo amewataka wataalam wa afya na lishe nchini kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kuhusuulaji unaofaa.
Mhe.Jenista ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kufuatia maadhinisho ya Lishe Kitaifa ambapo amesema Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku hiyo kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu manufaa ya Lishe bora na hatua madhubuti zinazopaswa kuchukuliwa na wananchi ili kuleta mabadiliko chanya.
Aidha amewataka wadau hao kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa afua za lishe katika ngazi zote ili kuhakikisha afua hizo muhimu zinatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia sera miongozo,kanuni na taratibu zilizopo na ameziagiza halmashauri nchini kuhakikisha fedha za utekelezaji wa afua za lishe ikiwemo uongezaji wa virutubishi kwenye vyakula,uhamasishaji wa elimu ya lishe kwa jamii ili kubaini matatizo ya utapiamlo.
Amesema lengo hilo litasaidia kupunguza tatizo la utapiamlo nchini kwa kuwa na jamii yenye afya bora kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambapo amesema uzingatiaji wa ulaji wa chakula ni muhimu kwa kila mmoja kwani jamii bado inakabiliwa na changamoto ya utapiamlo unaojumuisha lishe pungufu ikiwemo udumavu,ukondefu na uzito pungugu kwa watoto.
Mhe.Jenista ameongeza kuwa utapiamlo hudhoofisha makuzi ya watoto kimwili na kiakili na huongeza hatari ya magonjwa na gharama kubwa za matibabu kwani huathiri ubunifu na uwezo wa kufanya maamuzi wakati wa utu uzima,hupunguza tija na uzalishaji mali hali inayosababisha kuwa ni kikwazo kikubwa katika ustawi wa jamii na maendeleo kiuchumi.
Ameongeza kwa kusisitiza ulaji wa matunda,mbogamboga na vyakula vya asili ya wanyama kwa wingi ambavyo kwa kiasi kikubwa jamii haivitumii mara kwa mara,sambamba na kutumia vyakula vilivyoongezwa virutubisho ili kuepuka utapiamlo wa upungufu wa vitamini na madini mwilini pamoja na kuepuka ulaji wa vyakula vya mafuta,sukari,chumvi nyingi.
Ameeleza kuwa Mikoa ambayo imekuwa ikizalisha chakula kwa wingi ndiyo mikoa ambayo imekuwa haifanyi vizuri katika lishe bora kutokana na kutoongeza virutubishi kwenye vyakula wanavyopika.
Amebainisha kuwa kila mwaka serikali imekuwa ikitenga shilingi bilioni 5 ili ziweze kusaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yasiyoyakuambukiza
Kauli mbiu ya mwaka huu ya Mchongo ni afya yako zingatia unachokula, kauli mbiu hiyo inakumbusha afya bora ni nguzo muhimu ya mafaniko katika maisha ya mwanadamu ambapo kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya maamuzi tunayofanya kila siku kuhusu aina ya vyakula vinavyoliwa wa kuwalisha watoto.
Post A Comment: