Elizabeth Joseph, Arusha.

Wazazi na Walezi wametakiwa kuwekeza katika kutengeneza vijana wa kiume wacha Mungu kwa kupenda Ibada ili kutengeneza Kanisa lenye nguvu ya Mungu kwa baadae.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Kkkt Dayosisi ya Kaskazini Kati Mwalimu Loshilu Sambweti akimuwakilisha Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt,Godson Abel Mollel wakati wa Ibada maalum ya Harambee ya 12 ya  Ujenzi wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika Tarajali wa Mianzini jijini Arusha ambapo hadi sasa ujenzi wake umegharimu Milioni 434,804,000.

Amesema kuwa Kanisa la sasa limekuwa na upungufu wa Vijana wakiume pamoja na Wakina baba kushiriki Ibada mbalimbali kwenye makanisa tofauti na jinsia ya kike jambo alilosema linatakiwa kuhimizwa Sasa ili kuongeza idadi ya kundi hilo kwa baadae.

"Ukiangalia kwenye Kwaya wanawake ni wengi kuliko wanaume vivyo hivyo hata katika Ibada za kawaida tu idadi ya wanaume na vijana wakiume ni ndogo sana kuliko wakike,hali hii ikiendelea huko mbeleni tutakuja kukosa jinsia ya kiume kwenye makanisa yetu hivyo ni wajibu wetu Wazazi na Walezi kuhamisha wakina baba na watoto wetu wa kiume kumpemda Mungu na kupenda Ibada ili kuwa na Kanisa bora la kesho lenye kumcha Mungu"Amongeza kusema Mwalimu Sambweti.

Aidha aliagiza Viongozi wa Makanisa na Wakristo kuhakikisha wanawakumbuka wenye mahitaji  hasa wanaoishi pembezoni mwa miji kwakuwa wamekuwa wakiishi mazingira magumu tofauti na wanaoishi mijini.

"Wapo watu wanaabudu chini ya miti lakini wapo watumishi wa Mungu ambao hawana mavazi,viatu,wanatembea kwa miguu umbali mrefu kufanya Injili hivyo sisi tunaoishi mjini walau tunatembelea usafiri,tunaabudu mahali pazuri ni muhimu basi tuwakumbuke wenzetu wenye uhitaji kwa Sadaka mbalimbali kwa kufanya hivyo ni kuonesha upendo"Ameeleza Mwalimu Sambweti.

Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi wa Kkkt Usharika Tarajali wa Mianzini Mch,Yesse Solomoni Mushi aliwashukuru waumini na Viongozi wengine wa Kanisa hilo kwa kujitoa kwao katika kujenga Kanisa hilo la kisasa na kuwaomba wasichoke kumtolea Mungu katika kujenga nyumba yake.

"Kipekee nimshukuru Baba Askofu Mheshimiwa Dkt,Godson Abel Mollel kwa kukubali kushiriki nasi katika Ibada hii na kutoa mchango wake katika kufanikisha umaliziaji wa jengo hili lakini pia shukrani ziende kwa kila aliyejitoa kujenga nyumba hii ya Bwana ikiwemo wakristo wa Usharika huu,niombe tusichoke kumtolea Mungu kwa moyo mmoja"Amefafanua Mchungaji Yesse.

Ujenzi wa Kanisa hilo la kisasa ulianza rasmi mwaka 2015 na katika Harambee hiyo Jumla ya fedha taslimu shilingi Milioni 63,168,000 zilikusanywa huku shilingi Milioni 15,181,000 ikiwa ni ahadi ambapo lengo ni kukusanya Milioni 200 ili kumaliza kazi ya Ujenzi iliyobaki ikiwa ni ni pamoja na kupiga plasta,kumaliza ujenzi wa ukuta,kuweka mfumo wote wa umeme pamoja na madirisha na milango yote

Share To:

Post A Comment: