Kampuni ya ZARA Adventure, iliyoko Moshi mkoani Kilimanjaro, imezindua kampeni ya Twenzetu Kileleni season 4 kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa ZARA Adventure Bi.Zainabu alielezea lengo la kampeni hiyo na jinsi inavyolenga kuchochea utalii wa ndani na kukuza uhusiano kati ya jamii za wenyeji na watalii. Alisisitiza umuhimu wa kuenzi historia na utamaduni wa nchi yetu kupitia shughuli za utalii.

Kampeni ya Twenzetu Kileleni season 4 inajumuisha safari za kipekee kwenda katika Mliima mrefu Afrika,Mlima Kilimanjaro,

Aidha Bi Zainabu amesema kuwa washiriki wa kampeni hii watapata fursa ya kufurahia maajabu ya asili na utamaduni wa nchi yetu wakati wanapopanda mlima Kilimanjaro

Kwa upande wake Mgeni rasmi wa tukio hilo Bw. Salim Kikeke ameeleza kuwa kampeni ya Twenzetu Kileleni pia ina lengo la kusaidia katika kukuza uchumi wa jamii za wenyeji na kuhifadhi mazingira wakati wa shughuli za utalii.

Sambamba na hilo Bw. Kikeke amemshukuru Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya filamu ya Royal Tour,ambayo imepelekea ongezeko la watalii wa kigeni Nchi Tanzania.

Uzinduzi wa kampeni ya Twenzetu Kileleni season 4 ulikuwa ni mwanzo wa msisimko mpya katika sekta ya utalii nchini Tanzania. Kampeni hii inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika utalii wa ndani na kuchangia katika maendeleo ya jamii za wenyeji.



Share To:

Post A Comment: